Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Flatei Gregory Massay
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mbulu Vijijini
Primary Question
MHE. FLATEI G. MASSAY aliuliza:- Kutokana na sera ya Serikali kujenga vituo vya afya kila kata. Je, ni lini Serikali itajenga vituo hivyo katika Kata za Maretadu, Maghangw, Endamilay, Dinamu, Geterer, Masieda na kupandisha hadhi Zahanati ya Hayderer kuwa Kituo cha Afya?
Supplementary Question 1
MHE. FLATEI G. MASSAY: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana pamoja na majibu haya ya Serikali Jimbo la Mbulu Vijijini lina Kata 18 na tuna kituo kimoja tu cha afya na kama alivyosema kwamba tumetenga maeneo na wananchi wameshakusanya material yaani mchanga, simenti na wengine tumeanza kujenga, je, Serikali itaongeza nini katika jitihada hizi za wananchi ambao wenyewe wameamua kujenga vituo vya afya? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili kwa kuwa wamekiri kwamba Zahanati ya Hayderer miundombinu yake haifai ili zahanati ile ikahuishwe ikawa kituo cha afya, je, uko tayari sasa kuja pale ili kuangalia namna gani na kutusaidia ili tukapata walau kituo cha pili katika Jimbo la Mbulu Vijijini? (Makofi)
Name
Josephat Sinkamba Kandege
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kalambo
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, kama ambavyo nimejibu katika majibu yangu ya msingi tunakubaliana kabisa na jithada zinazofanywa na wananchi katika kujiletea maendeleo ikiwa ni pamoja na ujenzi wa vituo vya afya kama kazi nzuri ambayo imeanzishwa na wananchi wa Jimbo la Mheshimiwa Flatei.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kipekee naomba nichukue fursa hii kumpongeza na kumshukuru Mheshimiwa Flatei Massay jinsi ambavyo amekuwa akipigania wananchi wake kuhusiana na suala zima la afya, na sisi Serikali kwa kuunga mkono ndio maana katika hospitali 67 za Wilaya ambazo zinajengwa na wao ni wanufaika. Naomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwa kadri bajeti itakavyokuwa inaruhusu na hasa kwa wananchi ambao tayari wameonesha jitihada zao katika kujenga vituo vya afya na zahanati sisi kama Serikali tutakuwa tayari kwenda kushirikiana na wananchi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini juu ya utayari wangu hata kabla yeye hajasema anajua kwamba mimi niko tayari kwenda kule kwake ili tuende tukaone kitu gani kiko site tuweze kushauri namna bora ya kuweza kupeleka huduma kwa wananchi.
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved