Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Maryam Salum Msabaha

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. MARYAM SALUM MSABAHA aliuliza:- Baadhi ya Kambi za Jeshi la Wananchi nchini (JWTZ) zina majengo chakavu sana ikiwemo Kambi ya Nyuki Zanzibar:- Je, ni lini Serikali itatenga fedha za kutosha kwa ajili ya ujenzi wa Kambi hizi?

Supplementary Question 1

MHE. MARYAM S. MSABAHA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Naona Mheshimiwa Naibu Waziri sijui alikuwa kalala, naomba kuuliza maswali mawili ya nyongeza.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa Kambi hii niliyoitaja hasa hii Mesi ya Ulinzi na Usalama ipo katika mazingira ambayo siyo rafiki sana na jamii iliyowazunguka, upande kuna Skuli ya SOS na upande kuna Msikiti, pia kunakuwa na vitendo ambavyo vinaendelea pale ambavyo siyo rafiki na jamii inayowazunguka. Je, ni lini Serikali itahakikisha inatenga fedha za kutosha ili kukarabati Kambi hii na hasa hii Mesi ya Jeshi?
Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, kwa kuwa vikosi vingi vya Ulinzi na Usalama vinaishi uraiani na vinakuwa siyo rafiki sana na wananchi hasa wananchi ambao siyo waadilifu na nchi yao. Je, ni lini Serikali itahakikisha vikosi vyote vya Ulinzi na Usalama vinajengewa makazi bora na yenye sifa kama vikosi vya Ulinzi na Usalama?

Name

Eng. Hamad Yussuf Masauni

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kikwajuni

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI (K.n.y. WAZIRI WA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA): Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nimhakikishie Mheshimiwa Maryam Msabaha kwamba maoni yake tutayazingatia katika bajeti ya mwaka wa fedha ujao tutaangalia uwezekano wa kutilia maanani mapendekezo yake, hasa ukizingatia kwamba amezungumza changamoto ambazo ni za msingi kabisa .
Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusiana na nyumba, tayari kuna program ya ujenzi wa nyumba na hilo liko tayari katika mipango ya Serikali, nadhani muda siyo mrefu suala la nyumba litaanza kupunguzwa kadri ya uwezo wa nchi kifedha utakapokuwa unaruhusu.