Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Dr. Christine Gabriel Ishengoma
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA (K.n.y. MHE. BUPE MWAKANG’ATA) aliuliza:- Vijana wengi wamejiajiri katika shughuli mbalimbali ikiwemo waendesha bodaboda, lakini waendesha bodaboda hao wamekuwa wakisumbuliwa sana na askari wa barabarani kwa kutozwa faini ambazo muda mwingine hazina maana na hivyo kuwakatisha tamaa. Je, Serikali inachukua hatua gani ili kudhibiti vijana hawa wasinyanyaswe?
Supplementary Question 1
MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipatia nafasi, naomba niulize maswali mawili ya nyongeza.
Swali la kwanza, namshukuru Naibu Waziri amejibu vizuri lakini waendesha bodaboda hawa wengi hawana ujuzi wa Sheria na Kanuni za Barabarani. Je, kuna mkakati gani wa kuwapatia elimu hii ili kusudi waweze kuepukana na usumbufu na faini wanazozipata?
Swali la pili, kwa kuwa usafiri wa bodaboda unatoa usafiri kwa watu wengi lakini waendesha bodaboda hawa hawana leseni na hawana ujuzi wa kuendesha pikipiki hizi, kiasi kwamba wanasababaisha ajali nyingi na vifo.
Je, Serikali ina mpango gani wa kudhibiti tatizo hili? Ahsante sana.
Name
Eng. Hamad Yussuf Masauni
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kikwajuni
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI:
Mheshimiwa Spika, kuhusiana na suala la elimu kuna jitihada mbalimbali ambazo zinafanyika katika kutoa elimu kwa waendesha bodaboda. Miongoni mwa jitihada hizo ni kwanza Jeshi la Polisi limekuwa likitumia utaratibu wa kuwafuata kwenye vijiwe vyao hawa ambao wanaendesha bodaboda na kuwapa elimu, pia kupitia vipindi mbalimbali ambavyo vinaandaliwa kwenye television, kwenye radio na kupitia kwenye wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani ambavyo vinatumika kwa ajili ya kutoa elimu, kwa hiyo jitihada za kutoa elimu zinafanyika kwa kiwango kikubwa sana.
Mheshimiwa Spika, kuhusiana na swali lake la pili kwamba vijana ambao wanaendesha bodaboda bila leseni. Kwanza nichukua fursa hii kuendelea kusisitiza kwamba kuendesha bodaboda ama chombo chochote cha usafiri bila leseni ni kuvunja sheria na hivyo basi Jeshi la Polisi litaendelea kuwachukulia hatua wale wote ambao wanakiuka sheria za nchi katika eneo la usalama barabarani ikiwemo kuendesha bodaboda bila leseni. Kwa hiyo, nitoe wito kwa vijana wetu ambao hawana leseni kufuata taratibu za Kisheria ili waweze kujipatia leseni.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved