Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Mwanne Ismail Mchemba
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Tabora Mjini
Primary Question
MHE. MWANNE I. MCHEMBA (K.n.y. MHE. DKT. DALALY P. KAFUMU) aliuliza:- Gereza la Wilaya ya Igunga linakabiliwa na changamoto mbalimbali zikiwemo ukosefu wa ngome, hakuna Ofisi za Mkuu wa Gereza na Utawala, hakuna nyumba za askari lakini pia gereza hilo ni dogo na linahudumia wafungwa na mahabusu wa kiume tu, wafungwa na mahabusu wa kike hupelekwa Gereza Wilaya ya Nzega. Je, ni lini Serikali itajenga Gereza la Wilaya ya Igunga ili liweze kutoa huduma bora kwa wafungwa mahabusu Wilayani Igunga?
Supplementary Question 1
MHE. MWANNE I. MCHEMBA: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi na mimi niulize swali dogo la nyongeza.
Kwa kuwa, Serikali imekiri kutokuwa na nyumba ya mahabusu au kutokuwa na mahabusu ya wanawake katika Wilaya ya Igunga na kuwasababishia ndugu kutokuwasalimia na kutokujua afya zao kwa hao mahabusu ambao ni wanawake na kuwanyima haki zote.
Je, Serikali iko tayari kujenga mahabusu maalum ya wanawake kama dharura ili kuwaondolea adhabu wanayoipata wanawake na usumbufu wa kutoka Igunga kwenda Nzega mara kwa mara? Naiomba Serikali iangalie kwa jicho la huruma.
Name
Eng. Hamad Yussuf Masauni
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kikwajuni
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI:
Mheshimiwa Spika, nilizungumza wakati najibu swali la msingi kwamba ujenzi wa gereza hili ambao ulianza mwaka 2003 haujakamilika na nilisema kwamba utakapokuwa umekamilika basi changamoto ya mahabusu kwa wanawake itakuwa imepatiwa ufumbuzi. Kwa hiyo, nimuombe Mheshimiwa Mbunge astahamili wakati ambapo tunajiandaa kutafuta fedha kwa ajili ya kujenga gereza hili ili tuweze kupata ufumbuzi.
Mheshimiwa Spika, kuna jitihada ambazo tumeweza kuchukua katika baadhi ya maeneo mengine nchini ambapo tumeweza kutumia rasilimali za maeneo husika pamoja na wafungwa na nguvu na ushirikiano wa wananchi pamoja na Wabunge wa maeneo husika kuhamasisha katika ujenzi wa mabweni. Naomba nichukue fursa hii kumuahidi Mheshimiwa Mbunge kwamba nitafanya ziara rasmi katika gereza hili ili tushirikiane pamona na Mbunge wa Jimbo hilo kuona jinsi gani tunaweza tukafanya kutafuta njia za hatua za dharura kuweza kukabiliana na changamoto hii wakati tukisubiri fedha za bajeti za ujenzi wa gereza hili.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved