Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Suzana Chogisasi Mgonukulima

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. SUZANA C. MGONUKULIMA aliuliza:- Serikali inamhudumia Faru Fausta kwa gharama ya shilingi milioni 64 kwa mwezi na ambae hazalishi kutokana na kuwa ni mzee sana lakini Serikali hiyo haiwezi kumhudumia mwananchi aliyezeeka ambae hawezi kufanya shughuli zozote za kujikimu maisha na hana mtu wa kumsaidia. Je, ni kipi kilicho muhimu zaidi kwa Serikali kati ya Faru Fausta au mwananchi mzee asiyeweza kufanya lolote na hana wa kumsaidia?

Supplementary Question 1

MHE. SUZANA C. MGONUKULIMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kutokana na majibu ya Waziri naomba niulize maswali ya nyongeza kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa majibu ya Waziri, utunzwaji wa Faru Fausta umewezesha kulitumikisha taifa kwa gharama kubwa kuliko wazee wa Tanzania waliofanyakazi ya kuleta haki na amani katika Taifa hadi Faru Fausta kuonekana ni wa muhimu ni kwa ajili ya amani iliyopatikana kwa wazee hawa. (Makofi)
(a) Mheshimiwa Mwenyekiti, je, Serikali haioni ni wakati sasa wa kuhakikisha wazee wa taifa hili wanatunzwa kama vile gharama zote anavyotunzwa faru Fausta ili waweze kuleta amani katika nchi hii?
(b) Mheshimiwa Mwenyekiti, na kwa kuwa kwa majibu ya Waziri amesema anahifadhiwa na ana ulinzi mkali, hivyo hata watalii hawamuoni, hizo fedha za kigeni zinazopatikana zinatokana na nini na wakati amehifadhiwa? (Makofi)

Name

Japhet Ngailonga Hasunga (CPA)

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Vwawa

Answer

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza naomba niweke record vizuri kwa dada yangu Mheshimiwa Mbunge kwamba wanyama wana haki sawa kama binadamu wengine na huyu mnyama kutokana na uadimu wake, na kwamba ni moja ya wanyama ambao wapo hatarini kutoweka ndiyo maana tumemweka kwenye ulinzi maalum. Kutokana na umuhimu wake huo na kutokana na jinsi ambavyo ameliingizia Taifa fedha nyingi za kigeni na kutokana na kwamba watu wengi wanataka kujua maisha yake kwamba ataishi miaka mingapi, maana mpaka sasa hivi ana miaka 53 ndio maana tumeamua kumweka kwenye ulinzi huo sawa na binadamu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini sambamba na hilo Ilani ya Chama cha Mapinduzi inasema Wazee wote sasa hivi tunawatambua ili kutengeneza sera nzuri ya kuweza kuwasaidia na kuwalipa pensheni. Kwa hiyo, watalipwa sambamba na faru huyu, Faru Fausta ambaye ndiyo sera inavyosema ya Chama cha Mapinduzi, nashukuru. (Makofi)

NAIBU WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii naomba niongeze maelezo kidogo ya nyongeza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mujibu wa Sera ya Afya ya mwaka 2017 Serikali inatambua mchango na kuthamini mchango wa wazee na tumeweka utaratibu wazee wote ambao wako zaidi ya miaka 60 watapata matibabu bure.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tumeweka mkakati sasa hivi kuhakikisha kwamba wazee wanatambuliwa na kupewa vitambulisho vya kupewa matibabu na tumeweka utaratibu wa kuhakikisha kwamba, katika vituo vyetu vyote vya kutolea huduma za afya wazee wanapewa kipaumbele cha kwanza. (Makofi)
Kwa hiyo pamoja na majibu yote ambayo ametoa Naibu Waziri mchango huu ambao unapatikana katika mapato ya utalii katika sekta hii ya utalii ndio haya yanayoingia kwenye Mfuko Mkuu wa Taifa na kwenda kuwahudumia wazee hawa. (Makofi)