Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Halima Ali Mohammed

Sex

Female

Party

CUF

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. HALIMA ALI MOHAMMED aliuliza:- Je, Serikali imefanikiwa kwa kiasi gani kuimarisha majengo na vituo vya Polisi sanjari na kulipa madeni ya Wakandarasi waliojenga majengo hayo?

Supplementary Question 1

MHE. HALIMA ALI MOHAMMED: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Pamoja na majibu ya Mheshimiwa Naibu Waziri nina maswali mawili ya nyongeza:
(a) Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa yupo Mkandarasi ambaye amejenga makao Makuu ya Polisi Kusini Pemba pamoja na nyumba ya RPC kwa asilimia 100, vile vile amejenga Kituo cha Polisi cha Mkokotoni kwa asilimia 70, je, ni lini Serikali itamlipa Mkandarasi huyo?
(b) Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa Wakandarasi wako kibiashara zaidi na kwa kuwa muda aliojenga Mkandarasi huyu ni mrefu, je, sasa Serikali iko tayari kumlipa kwa thamani ya shilingi iliyoko sokoni sasa?

Name

Eng. Hamad Yussuf Masauni

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kikwajuni

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Naibu Spika, kama nilivyozungumza katika jibu langu la msingi ni kwamba, kila mwaka tunatenga bajeti kwa ajili ya maendeleo na katika fedha hizo, ndipo tunatumia sehemu ya fedha hizo kwa ajili ya kuwalipa Wakandarasi na Mkandarasi ambaye amejenga kituo cha Tumbatu na kituo hicho ambacho umekizungumza kilichopo Kusini Pemba ni miongoni mwa Wakandarasi mbalimbali ambao wanatudai, tutakuwa tukiwalipa. Mwaka huu katika Wakandarasi ambao tumepanga kuwalipa kiasi kitakachoweza kulipwa ni huyo ambaye amemzungumza Mheshimiwa Mbunge.