Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Boniphace Mwita Getere
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bunda
Primary Question
MHE. BONIPHACE M. GETERE aliuliza:- Kila mwaka wanyama waharibifu wamekuwa wanakula mazao ya wakulima katika Jimbo la Bunda na Serikali imekuwa ikitumia fedha nyingi katika kulipa fidia ya kifuta jasho na kifuta machozi kwa wakulima hao:- Je, Serikali ina mikakati gani ya kuzuia wanyama hao wakiwemo Tembo?
Supplementary Question 1
MHE. BONIPHACE M. GETERE: Mheshimiwa Spika, ahsante. Pamoja na majibu mazuri ya Serikali, naomba kuuliza maswali mawili ya nyongeza. Kwanza, niwapongeze Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kunipa gari la kusaidia kufukuza wanyama waharibifu kwenye maeneo yangu, lakini pia, najua wana mpango wa kupeleka fedha za kifuta jasho katika maeneo hayo.
Mheshimiwa Spika, swali la kwanza, kwa kuwa, sasa ni miaka 15 Vijiji vya Hunyali, Kihumbu, Maliwanda, Salakwa, Kyandege, Tingilima, wamekuwa ni wahanga wakuu wa wanyama waharibifu wa mazao, sasa Serikali ina mpango gani sasa mbadala ikiwepo kupima vijiji hivyo ili kupata Hati Miliki za Kimila na kuendesha maisha ya wananchi wa makazi hayo?
Mheshimiwa Spika, swali la pili, kwa kuwa sasa kuona ni kuamini na kuamini ni kuona, ni lini sasa Wizara au Waziri atatembelea maeneo haya, ili kujihakikishia hali halisi ya uharibifu huo? Mheshimiwa Spika, ahsante. (Makofi)
Name
Japhet Ngailonga Hasunga (CPA)
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Vwawa
Answer
NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Maliasili na Utalii, kwanza ni kweli kabisa kwamba, sasa hivi Wizara ina mpango mkubwa mahususi wa kuhakikisha kwamba vijiji vyote ambavyo vinazungukwa na Hifadhi za Taifa vinakuwa na mpango bora wa matumizi ya ardhi. Hili tunalifanya kuanzia mwaka wa fedha unaoanza Julai mwaka huu. Katika kutekeleza hilo tunashirikiana na Wizara ya Ardhi, ambapo ndiyo wamepewa hizi fedha kwa ajili kusaidia kupima vijiji vyote hivi ili wawe na mpango mzuri na kuhakikisha matumizi yanaeleweka vizuri kabisa.
Mheshimiwa Spika, swali lake la pili, kuhusu kwenda kutembelea na kujionea hali halisi, naomba nimwambie tu Mheshimiwa Mbunge kwamba tuko tayari wakati wowote mara baada ya Mkutano huu wa Bunge kumalizika tutapanga ni lini tunaweza kufika kule ili tujionee hali halisi ilivyo huko.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved