Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Machano Othman Said
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
House of Representatives
Primary Question
MHE. MACHANO OTHMAN SAID (K.n.y. MHE. USSI SALUM PONDEZA AMJADI) aliuliza:- Vijana wa Kitanzania wanakabiliwa na tatizo sugu la ukosefu wa ajira na hivyo nguvu kazi kupotea badala ya kutumika kwa uzalishaji:- (a) Je, Jeshi la Kujenga Taifa lina mpango gani wa kutumia nguvu kazi ya vijana kwa kuanzisha miradi ya kilimo cha kisasa ili kuondoa tatizo la ajira? (b) Je, ni vijana wangapi wamenufaika na ajira kwa kila mwaka kupitia Jeshi la Kujenga Taifa (JKT)?
Supplementary Question 1
MHE. MACHANO OTHMAN SAID: Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Waziri, naomba kuuliza swali moja la nyongeza, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, wakati wa uzinduzi wa Ukuta wa Mererani ambao Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliuzindua, Mheshimiwa Rais aliridhika sana na kazi ambayo imefanywa na Jeshi na kuahidi kwamba vijana 2,500 wa JKT ambao walishiriki katika ujenzi huo waajiriwe na vyombo vya ulinzi vya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Je, ni hatua gani ambazo zimefikiwa kuhusu ajira za vijana wale hadi hivi sasa?
Name
Dr. Hussein Ali Mwinyi
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kwahani
Answer
WAZIRI WA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA:
Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Machano Othman Said, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kwamba Mheshimiwa Rais alitoa ahadi ya kuwaajiri vijana walioshughulika katika ujenzi wa Ukuta pale Mererani. Zoezi hilo kwa kweli limeshaanza, polisi wamepokea vibali vya ajira, usaili umeanza na ni mategemeo yetu kwamba vyombo vingine vya ulinzi na usalama watakapokuwa wamepata vibali wataendelea kuwachukua vijana hawa.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved