Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Christopher Kajoro Chizza

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Buyungu

Primary Question

MHE. ENG. CHRISTOPHER K. CHIZA aliuliza:- Sera ya Serikali ni kuwa na Hospitali za Wilaya na Vituo vya Afya katika kila Kata:- • Je, ni lini Serikali itaanza ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Kakonko? • Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga Vituo vya Afya katika Kata za Kiziguzigu, Kasanda, Gwarama, Rugenge, Nyamutukiza na Kata nyingine ambazo hazina Vituo vya Afya?

Supplementary Question 1

MHE. ENG. CHRISTOPHER K. CHIZA: Mheshimiwa Spika, kwanza nashukuru kwa majibu mazuri ya Serikali. Naishukuru pia Serikali kwa kututengea Sh.500,000,000 za kujenga kituo cha Afya cha Gwanumpu na nimetoka Jimboni kazi sasa imeanza, ahsanteni sana.
Mheshimiwa Spika, hata hivyo sasa nina swali moja tu. Pamoja shukrani hizo, Mheshimiwa Waziri kwa kuwa anajua kabisa Ubunge wangu bado mbichi; sasa ananiahidi nini kwa awamu hii inayofuata; kwamba itaanza lini ili Kata za Kiziguzigu, Kasanda, Rugenge, Gwarama na Nyamtukuza nazo zipate fedha za kujenga vituo vya afya? (Makofi)

Name

Josephat Sinkamba Kandege

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kalambo

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE): Mheshimiwa Spika, kama ambavo tumeainisha kwenye ilani yetu ya CCM kwamba kila kata tutajenga kituo cha afya na kila Wilaya ambako hakuna Hospitali ya Wilaya tutaenda kujenga, naomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge, miongoni mwa maeneo ambayo tutahakikisha yanajengwa vituo vya afya ni yale ambayo yana upungufu mkubwa ikiwa ni pamoja na Wilaya yake ya Kakonko.
Mheshimiwa Spika, naomba nimuhakikishie, hakika pale ambapo bajeti itaweza kupatikana ikaongezeka hatutawasahau Kakonko na hasa tukiwa tunajibu fadhira ambazo wananchi wa Kakonko na hasa Buyungu walitoa kwa Chama cha Mapinduzi.

Name

Catherine Valentine Magige

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. ENG. CHRISTOPHER K. CHIZA aliuliza:- Sera ya Serikali ni kuwa na Hospitali za Wilaya na Vituo vya Afya katika kila Kata:- • Je, ni lini Serikali itaanza ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Kakonko? • Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga Vituo vya Afya katika Kata za Kiziguzigu, Kasanda, Gwarama, Rugenge, Nyamutukiza na Kata nyingine ambazo hazina Vituo vya Afya?

Supplementary Question 2

MHE. CATHERINE V. MAGIGE: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali dogo la nyongeza. Kwa kuwa tumekuwa tukishuhudia ujenzi wa Hospitali za Wilaya katika Mkoa wangu wa Arusha, Wilaya mbalimbali kama Longido, Monduli na nyinginezo na upanuzi mkubwa wa vituo vya afya ukiendelea, nataka kufahamu; Je, Serikali imejipangaje kuhakikisha wanaleta wataalam wa kutosha hasa wa dawa za usingizi ili wananchi wa Arusha wapate huduma, hasa ya mama na mtoto? (Makofi)

Name

Dr. Faustine Engelbert Ndugulile

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kigamboni

Answer

NAIBU WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO: Mheshimiwa Spika, Serikali imewekeza katika uboreshaji wa vituo vya afya takribani zaidi ya 300 nchi nzima. Hata hivyo tunatambua kwamba uboreshaji huu unaendana sambamba na kuongeza huduma za upasuaji. Sisi kama Serikali sasa hivi tumeshapeleka watumishi zaidi ya 200 kwenda kusomea masuala ya usingizi. Tunatumaini ndani ya muda mfupi huu watumishi wale watakuwa wamekamilisha mafunzo hayo na tutawasambaza katika vituo vya kutolea huduma.