Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Augustino Manyanda Masele
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mbogwe
Primary Question
MHE. AUGUSTINO M. MASELE aliuliza:- Serikali iliahidi kuanza utekelezaji wa mradi wa umeme wa ujazo (Densification) Mkoani Geita kuanzia mwezi Oktoba, 2018 lakini hadi sasa mradi huo haujaanza:- Je, ni lini mradi huo utaanza kutekelezwa katika Wilaya ya Mbogwe?
Supplementary Question 1
MHE. AUGUSTINO M. MASELE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri, napenda kuuliza maswali mawili madogo ya nyongeza. Hadi sasa Wilaya ya Mbogwe ni vijiji 28 tu ambavyo tayari vina umeme na REA awamu ya tatu inajumuisha vijiji 28 pia. Sasa hapa nataka kuuliza Serikali kama vile vijiji vya REA awamu ya tatu na vyenyewe vitahusishwa katika hii Densification?
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, vijiji 31 haviko kabisa katika mpango wa REA awamu ya tatu: Je, Serikali ina mpango gani wa kuhakikisha kwamba vijiji 31 vya Wilaya ya Mbogwe ambavyo havijapata umeme vinapatiwa umeme?
Name
Subira Khamis Mgalu
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa fursa ya kujibu maswali ya nyogeza ya Mheshimiwa Masele. Maswali yake mawili yalijielekeza kwanza kwenye mradi unaendelea wa REA awamu ya tatu katika vijiji 28. Alikuwa anauliza je, huu mradi wa ujazilizi utafika katika maeneo hayo?
Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Mbunge ametaja kwamba katika Jimbo lake kuna vijiji 28 vina umeme na anaamini katika vijiji hivyo vipo Vitongoji ambavyo havikuguswa katika miradi ya REA awamu ya kwanza na awamu ya pili. Kwa hiyo, nataka nimtaarifu Mheshimiwa Mbunge kwamba mradi wa ujazilizi utaelekea kwenye maeneo yale ya vijiji 28 ambapo kuna Vitongoji havikufikiwa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali lake la pili Mheshimiwa Mbunge ameulizia vijiji 31 katika Jimbo lake ambavyo havina umeme. Nataka nilitaarifu Bunge lako Tukufu na wananchi wa Jimbo la Mbogwe ambapo Mheshimiwa Mbunge anafanyia kazi nzuri kwamba vijiji 31 vitaingia kwenye mradi wa REA awamu ya tatu mzunguko wa pili na sasa kazi hiyo imeanza na ameshapokea hiyo orodha na mchakato unaendelea na mradi huu unatarajia kuanza mwezi Julai, 2019 ahsante.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved