Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Ruth Hiyob Mollel
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. RUTH H. MOLLEL (K.n.y. MHE. NAGHENJWA L. KABOYOKA) aliuliza:- SUMA-JKT Idara ya Zana za Kilimo ilikopesha 5,355,153,000/= kwa idara mbalimbali ndani ya SUMA-JKT. Taarifa za CAG zimeonesha kuwa hadi kufikia tarehe 30 Juni, 2016 ni kiasi cha Sh.534,785,000/= ambayo ni kiasi chini ya asilimia 10 ndio kilirejeshwa:- (a) Je, ni kiasi gani hadi sasa kimerejeshwa kwenye Idara hiyo ya Zana za Kilimo? (b) Je, Serikali itakubaliana na mimi kwamba, uzembe huu wa kutohakikisha mikopo ya fedha za Serikali inarudishwa kwa wakati ili wakulima wengine nao waweze kukopeshwa kumechangia kukwamisha juhudi za kupunguza umaskini nchini? (c) Je, Serikali inachukua hatua gani kuwawajibisha waliohusika na utoaji huo wa mikopo bila kuhakikisha inarudishwa kwa wakati?
Supplementary Question 1
MHE. RUTH H. MOLLEL: Mheshimiwa Mwenyekiti, asante kwa kunipa nafasi ya kuuliza maswali mawili ya nyongeza. Pesa hizo zilizokwenda kununua hayo matrekta ni pesa za walipakodi wa nchi hii na ni nyingi sana na mpaka sasa hivi karibu 2.9 billion hazijarejeshwa. Mkakati mahususi a kuhakikisha kwamba, hii pesa inarudi, ni upi?
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, ni kwa nini sasa wale wote ambao walikopa haya matrekta majina yao yasiwekwe kwenye magazeti tuwajue ni akinanani hao wanaokwamisha kurudisha mikopo ya Serikali? (Makofi)
Name
Dr. Hussein Ali Mwinyi
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kwahani
Answer
WAZIRI WA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Ruth Mollel, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, kama nilivyosema katika jibu langu la msingi ni kwamba, fedha zilizokuwa zimekopeshwa ni bilioni tano na kitu ambazo zimesharudishwa ni bilioni mbili, yani tuko kwenye asilimia 45 ya urejeshaji, maana yake ni jitihada kubwa zimefanyika hapo na kiwango kilichobaki kitarejeshwa kwa sababu, fedha hizi hawajakopeshwa watu nje, zimekopeshwa ndani ya Mashirika ya SUMA-JKT lenyewe kwa maana hiyo wanafanya biashara mbalimbali. Sina shaka kabisa kwamba, fedha hizi zote zitarudi na faida itapatikana kwa sababu, SUMA-JKT limejiwezesha kimtaji kuanzisha biashara nyingine.
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili kuhusu majina ya waliokopa matrekta kwamba, yawekwe kwenye magazeti. Jambo hili lilishafanyika, majina yaliwekwa kwenye magazeti na fedha hizi zimeendelea kukusanywa. Naomba nitoe taarifa kwamba, tokea Mheshimiwa Rais ametoa kauli ya kwamba, watu wote waliokopa warejeshe, tayari wamekusanya bilioni mbili na milioni 900.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaendelea na jitihada hizi na kama tulivyosema SUMA-JKT itaanza kuuza mali za walikopa endapo hawatarejesha baada ya kukamilika kwa zoezi la ukusanyaji wa madeni.
Name
Abdallah Majurah Bulembo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Nominated
Primary Question
MHE. RUTH H. MOLLEL (K.n.y. MHE. NAGHENJWA L. KABOYOKA) aliuliza:- SUMA-JKT Idara ya Zana za Kilimo ilikopesha 5,355,153,000/= kwa idara mbalimbali ndani ya SUMA-JKT. Taarifa za CAG zimeonesha kuwa hadi kufikia tarehe 30 Juni, 2016 ni kiasi cha Sh.534,785,000/= ambayo ni kiasi chini ya asilimia 10 ndio kilirejeshwa:- (a) Je, ni kiasi gani hadi sasa kimerejeshwa kwenye Idara hiyo ya Zana za Kilimo? (b) Je, Serikali itakubaliana na mimi kwamba, uzembe huu wa kutohakikisha mikopo ya fedha za Serikali inarudishwa kwa wakati ili wakulima wengine nao waweze kukopeshwa kumechangia kukwamisha juhudi za kupunguza umaskini nchini? (c) Je, Serikali inachukua hatua gani kuwawajibisha waliohusika na utoaji huo wa mikopo bila kuhakikisha inarudishwa kwa wakati?
Supplementary Question 2
MHE. ALHAJI ABDALLAH M. BULEMBO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Pamoja na jibu zuri la Mheshimiwa Waziri mhusika, kuna viongozi wa Serikali na hata humu Bungeni waliokopa SUMA katika matrekta hayo. Mheshimiwa Waziri licha ya kuwatangaza wamefikishwa kwa Spika ili tutangaziwe humu Bungeni tujue ni wapi wanaodaiwa?
Name
Dr. Hussein Ali Mwinyi
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kwahani
Answer
WAZIRI WA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Bulembo, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kwamba wako viongozi wa Serikali na baadhi ya Wabunge waliokopa matrekta haya. Juhudi tulizozifanya ni kwamba, tuliziandikia mamlaka za ajira za kila mmoja, kwa hivyo, Mheshimiwa Spika anayo orodha ya Wabunge na Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya waliohusika tumeandika barua TAMISEMI na Wizara zote kwa ujumla, kila mamlaka ya ajira imeandikiwa barua. Ni mategemeo yangu kwamba, kila mamlaka ya ajira itachukua hatua stahili ili kuweza kuzipata fedha hizi.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved