Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Allan Joseph Kiula
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Iramba Mashariki
Primary Question
MHE. ALLAN J. KIULA aliuliza:- Pamoja na mambo mengine, Sera ya Serikali ya Awamu ya Tano imelenga kuongeza asilimia za upatikanaji wa maji vijijini. (a) Je, lini Serikali itafanya utafiti wa vyanzo vya maji katika Jimbo la Mkalama ili kuwa na uhakika wa rasilimali hiyo? (b) Je, lini Serikali itatoa fedha za kutosha kuwapatia maji safi wananchi wa Jimbo la Mkalama?
Supplementary Question 1
MHE. ALLAN J. KIULA: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa kunipa tena nafasi. Naomba kuuliza maswali mawili ya nyongeza ikiwemo kushukuru ziara ya Makamu wa Rais ambaye alibaini ubadhirifu wa mradi wa Nyahaa, natumaini Wizara inaendelea kulifanyia kazi suala hilo. Swali la kwanza, je, Serikali iko tayari kuongeza fedha za utafiti hususan katika maeneo yasiyo na miradi mikubwa kama ile iliyopitiwa na maji ya Ziwa Victoria au mkopo wa India ikiwemo Mkalama ili kuweza kupata vyanzo vya uhakika vya maji?
Mheshimiwa Spika, swali la pili je, ni kweli Serikali inatekeleza miradi hiyo na pesa hizo zilitengwa, je ni lini certificate za wakandarasi zitalipwa ili kazi iweze kuendelea kwa sababu kazi kule imesimama kutokana na wakandarasi kutokulipwa?
Name
Jumaa Hamidu Aweso
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Pangani
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, awali ya yote kwanza nimpongeze Mheshimiwa Allan Kiula Mbunge wa Jimbo la Mkalama kwa kazi nzuri sana anayoifanya katika jimbo lake. Kubwa ni kuhusu suala zima la utafiti, sisi kama Serikali tunautambua umuhimu wa suala zima la utafiti hasa katika sekta ya maji kwa sababu italeta mapinduzi makubwa. Nataka nimhakikishie sisi kama Serikali hatutokuwa kikwazo kuongeza fedha za utafiti kadiri bajeti itakavyokuwa imeruhusu katika kuhakikisha kwamba tunakuwa na tafiti ambazo zitaruhusu kufanya mapinduzi katika sekta ya maji.
Mheshimiwa Spika, lakini kuhusu suala zima la madai ya wakandarasi hususan katika miradi ya jimbo lake. Utekelezaji wa miradi ya maji unategemeana na fedha, tukubali tulikuwa na madai zaidi ya bilioni 88 ya wakandarasi lakini tunashukuru Wizara ya Fedha ijumaa imetupa zaidi ya bilioni 44 kwa ajili ya kuwalipa wakandarasi certificate zao na wametupa commitment ndani ya mwezi huu wa nne watatupa bilioni 44 zingine kwa ajili ya kuwalipa wakandarasi fedha zao.
Nataka nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge apate nafasi ya kuwasiliana na sisi katika kuhakikisha tunamlipa mkandarasi wake ili aweze kuendeleza miradi ya maji katika Jimbo lake la Mkalama.
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved