Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Juma Othman Hija
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tumbatu
Primary Question
MHE. JUMA OTHMAN HIJA Aliuliza:- Miongoni mwa malengo ya Benki ya TPB ni kupeleka huduma ya kibenki kwenye maeneo ya vijijini na pembezoni ambayo hayafikiwi na huduma hizo:- Je, ni kwa kiasi gani lengo hilo limefikiwa mpaka kufikia mwaka 2018?
Supplementary Question 1
MHE. JUMA OTHMAN HIJA: Mheshimiwa Spika, ahsante, namshukuru Mheshimiwa Waziri kwa majibu yake mazuri na ya kutoshereza kabisa, lakini nina swali moja la nyongeza.
Majibu yake yamejikita sana kwenye maeneo ya miji, swali langu ni kwamba Serikali ina mpango gani, huduma hizi kuzipeleka katika visiwa vidogovidogo kama vile Tumbatu?
Name
Dr. Ashatu Kachwamba Kijaji
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Kondoa
Answer
NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Spika, kama nilivyosema huduma zetu za TPB zimeongezeka kwa kiwango kikubwa na tumeweza kuwafikia wananchi walio wengi na kwa visiwa vyetu kwa Zanzibar tumeshafungua matawi tayari na sasa tunajipanga kwenda kufungua katika visiwa hivi vidogo, wakati huo tukiendelea kuwahudumia kwa kupitia mfumo wa kidigitali.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved