Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Dr. Shukuru Jumanne Kawambwa

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bagamoyo

Primary Question

MHE. DKT. SHUKURU J. KAWAMBWA aliuliza:- Kufuatia majibu ya Swali langu Na. 17 lililojibiwa tarehe 07/11/2018 kuhusu Bagamoyo kupata hadhi ya Halmashauri ya Mji, Serikali ilielekeza kwamba tusubiri wasilisho la Kamati ya ushauri ya Mkoa wa Pwani (RCC) ili Ofisi ya Rais (TAMISEMI) iweze kulifanyia kazi ombi hilo; na suala hilo limeshajadiliwa na RCC na taarifa kuwasilishwa Ofisi ya Rais (TAMISEMI):- Je, ni lini sasa Serikali itaipa Bagamoyo hadhi ya kuwa Halmashauri ya Mji?

Supplementary Question 1

MHE. DKT. SHUKURU J. KAWAMBWA: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kunipa fursa hii ya kuuliza swali moja la nyongeza na nashukuru kwa majibu mazuri ya Mheshimiwa Waziri. Kwa kutambua kwamba tangu mwaka 2005 miaka 14 sasa wakati ambapo Bagamoyo ilipewa hadhi ya mamlaka ya Mji Mdogo uongozi na wananchi wa Bagamoyo wameendelea kupambana kutekeleza vigezo 12 vya kupandisha hadhi mji ule kuwa halmashauri ya mji. Mpaka hivi sasa imebaki vipengele hivyo viwili kimoja cha master plan kingine cha upimaji.

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa tutaendelea kupambana na hiki cha master plan lakini upimaji wa ardhi ni suala ambalo linahitaji gharama kubwa. Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo haina vitendea kazi vya upimaji wa ardhi hivi sasa havina vyombo kwa ajili ya upimaji wa ardhi. Je, Serikali ina kauli gani kuweza kuisaidia halmashauri hii ambayo imepambana miaka 15 sasa kwa ajili ya kuweza kupata hadhi?

Name

Dr. Selemani Said Jafo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kisarawe

Answer

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nampongeza Mheshimiwa Dkt. Jumanne Shukuru Kawambwa yeye na viongozi wake na wenzake na Mwenyekiti wa Halmashauri waliweza kufika ofisini mara kadhaa katika jambo hilo. Tunafahamu kwamba juhudi kubwa inafanyika na ni azma yetu kuhakikisha kwamba maeneo yote ambayo yana kipaumbele tuweze kuyafanyia kazi. Katika jambo hili naomba niseme wazi kweli tumekuwa na changamoto katika suala zima la upatikanaji wa vifaa lakini hata hivyo niwashukuru sana wenzetu wa Wizara ya Ardhi kwa ushirikiano mkubwa tunaoendelea kuufanya.

Mheshimiwa Naibu Spika, hivi sasa halmashauri mbalimbali zitaweza kupata vifaa hivi kwa ajili ya kuhakikisha kwamba hivi vifaa vya upimaji vinaweza vikapatikana na tukumbuke wazi hata katika bajeti ya Wizara ya Ardhi jambo hili waliainisha wazi. Kwa hiyo, naomba nimhakikishie Mheshimiwa Jumanne Shukuru Kawambwa kwamba Serikali inalichukua hili kwa uzito mkubwa sana kuhakikisha halmashauri zetu zinawezeshwa kuhakikisha zinapima maeneo yao kwa urahisi zaidi ahsante.