Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Juma Kombo Hamad
Sex
Male
Party
CUF
Constituent
Wingwi
Primary Question
MHE. JUMA KOMBO HAMAD aliuliza:- Watu wanaoishi na VVU wanapata shida sana katika kupata lishe bora na matibabu ya uhakika:- (a) Je, Serikali imejipangaje katika kuwapa mikopo itakayowasaidia kuendesha maisha yao kupitia vikundi mbalimbali? (b) Je, kwa nini Serikali isione umuhimu wa kutenga sehemu ya mapato ya ndani ya Halmashauri kwa ajili ya kundi hilo?
Supplementary Question 1
MHE. JUMA KOMBO HAMAD: Mheshimiwa Spika, ahsante. Serikali kwa muda mrefu imekuwa ikitegemea fedha kutoka kwa wafadhili katika kuhudumia waathirika wa gonjwa la UKIMWI fedha ambazo upatikanaji wake umekuwa na changamoto kubwa. Nilitaka kujua tu, Serikali ina mkakati gani kuhakikisha kwamba sasa inatenga fedha za ndani katika kuhudumia kundi hili la wagonjwa wa UKIMWI? Ahsante. (Makofi)
Name
Dr. Faustine Engelbert Ndugulile
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kigamboni
Answer
NAIBU WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO: Mheshimiwa Spika, ni kweli Serikali imekuwa inashirikiana na wadau katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa UKIMWI na wadau wakubwa ni pamoja na Global Fund na PEPFA.
Mheshimiwa Spika, katika kuliona hilo na kwa lengo la kuhakikisha kwamba hizi huduma za matibabu au huduma afua za VVU kwa waathirika zinakuwa endelevu, Serikali imeanzisha Mfuko wa Masuala ya UKIMWI ambao unaitwa AIDS Trust Fund ambapo Serikali inaweka fedha pale, inachangia fedha zake kwa lengo la kuhakikisha kwamba baadhi ya afua zinakuwa funded kwa kupitia mfuko huo.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved