Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Sikudhani Yasini Chikambo
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. SIKUDHANI Y. CHIKAMBO (K.n.y. MHE. TAUHIDA CASSIAN GALLOS) aliuliza:- Je, Serikali haioni umuhimu wa kufunga Kamera ndani ya Vituo vya Polisi sasa ili kupunguza malalamiko kwa baadhi ya wananchi wanapohudumiwa kwa kumwezesha Mkuu wa Kituo kufuatilia mwenendo wa shughuli za Kituo akiwa Ofisini au kwa kutunza kumbukumbu za matukio yanayotokea kwenye vituo hivyo?
Supplementary Question 1
MHE. SIKUDHANI Y. CHIKAMBO: Mheshimiwa Spika, ahsante. Kwanza napenda kumpongeza Naibu Waziri kwa majibu yake mazuri; lakini kama ilivyoelezwa kwenye swali la msingi kwamba kumekuwa na malalamiko mengi katika Vituo vyetu vya Polisi pale wananchi wetu wanapokwenda kuhudumiwa katika maeneo yale:
Sasa je, ni mkakati gani wa Serikali katika kuhakikisha siku zijazo kunafungwa CCTV Camera katika hayo maeneo ili kuleta ushahidi katika yale matukio wanayofanyiwa wananchi pale? (Makofi)
Mheshimiwa Spika, ninafahamu kwamba Serikali ina dhamira ya dhati katika kuhakikisha Jeshi la Polisi linafanya vizuri, lakini kama litafanya vizuri bila kutunza kumbukumbu haitasaidia. Ni lini sasa mkakati wa Serikali katika kuhakikisha matukio yote yanakuwa katika kumbukumbu ili linapohitajika jambo lolote kwa mtuhumiwa yeyote linapatikana kwa urahisi? Ahsante. (Makofi)
Name
Eng. Hamad Yussuf Masauni
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kikwajuni
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Spika, nampongeza Mheshimiwa Sikudhani Chikambo kwa maswali yake mazuri. Nimhakikishie kwamba kama ambavyo nimejibu katika jibu la msingi, ni kwamba dhamira hiyo Serikali kupitia Jeshi la Polisi ya kufanya maboresho katika mfumo mzima wa TEHAMA ikiwemo maeneo mawili ambayo ameyazungumza ya mifumo ya CCTV na kumbukumbu kwa kutumia teknolojia ya kisasa, dhamira hiyo ipo na pale ambapo bajeti itaruhusu, basi sisi tutakamilisha huo mpango.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved