Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Neema William Mgaya
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. NEEMA W. MGAYA (K.n.y. MHE. DEO K. SANGA) aliuliza:- Askari wa Kituo cha Polisi katika Mji wa Makambako hawana gari la doria wala nyumba za kuishi:- (a) Je, ni lini Serikali itajenga nyumba za kuishi Askari hao? (b) Je, ni lini Serikali itatoa gari la doria kwa Kituo cha Polisi Makambako?
Supplementary Question 1
MHE. NEEMA W. MGAYA: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuweza swali la nyongeza. Kwanza naipongeza Serikali kwa jitihada kubwa walizozifanya katika Jimbo la Makambako, lakini vilevile eneo la Polisi la Makambako lilipimwa na kufanyiwa uthamini kwa ajili ya kulipa fidia wananchi ambao walikuwepo ndani ya eneo hilo.
Mheshimiwa Spika, nataka kujua, lini Serikali itawalipa wananchi hawa pesa zao kama fidia?
Mheshimiwa Spika, swali la pili; Wilaya ya Wanging’ombe tuna changamoto ya Kituo cha Polisi; nichukue nafasi hii kulipongeza Kanisa Katoliki kwa kuona umuhimu wa usalama wa raia na kujitolea baadhi ya majengo kutumika kama Kituo cha Polisi ndani ya Wilaya yetu ya Wanging’ombe. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, vilevile Halmashauri ya Wilaya ya Wanging’ombe imeshatoa kiwanja, nilitaka kujua: Je, lini Serikali itajenga Kituo hiki cha Polisi ndani ya Wilaya yetu ya Wanging’ombe?
Name
Eng. Hamad Yussuf Masauni
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kikwajuni
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Spika, kuhusiana na fidia ya wananchi, nataka nimjulishe Mheshimiwa Mbunge kwamba tumeamua kuwaachia hilo eneo wananchi, kwa hiyo, suala la fidia halipo tena.
Mheshimiwa Spika, kuhusu suala la Kituo cha Polisi, niwapongeze Kanisa kwa kuanzisha hizo jitihada pamoja na wananchi wa eneo hilo; na niwahakikishie kwamba pale ambapo hali itaruhusu tutaongezea nguvu jitihada hizo ili Kituo hicho kiweze kukamilika. Tunatambua umuhimu wa Kituo hicho.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved