Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Mattar Ali Salum
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Shaurimoyo
Primary Question
MHE. MATTAR ALI SALUM aliuliza:- Miongoni mwa kero za Muungano ni wananchi wa Zanzibar waletapo magari yao Tanzania Bara kutoruhusiwa kutembea mpaka yabadilishwe namba, wakati magari yanayotoka Bara yafikapo Zanzibar yanaruhusiwa kutembea kwa muda wote bila ya bughudha yoyote:- (a) Je, Serikali inalifahamu suala hili? (b) Kama ndiyo, je, Serikali ina mpango gani madhubuti wa kutatua suala hili ili Watanzania waendelee kufaidi matunda ya Muungano?
Supplementary Question 1
MHE. MATTAR ALI SALUM: Mheshimiwa Mwenyekiti, nimshukuru Mheshimiwa Naibu Waziri, ameeleza suala la sheria tofauti. Nimfahamishe Kenya na Tanzania tuna sheria tofauti, Uganda na Tanzania kuna sheria tofauti lakini bado magari ya Kenya yanapewa kibali kwa urahisi kuweza kutembea Tanzania Bara lakini magari yanayotoka Zanzibar mpaka uweke deposit (pesa nyingi) ambapo ndiyo unaweza kupewa kibali cha kutembelea Tanzania Bara. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa nimuulize Mheshimiwa Waziri wana utaratibu gani utakaokuwa rahisi kuweza kusaidia watu wa Zanzibar kuweza kutembelea gari ndani ya Tanzania Bara? Ahsante. (Makofi)
Name
Dr. Ashatu Kachwamba Kijaji
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Kondoa
Answer
NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kujibu swali moja la Mheshimiwa Mattar, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, utaratibu rahisi uliopo ni huo uliopo sasa mpaka pale sheria nilizozieleza kwenye jibu langu la msingi zitakaporekebishwa kwa pamoja.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved