Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Ritta Enespher Kabati

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. RITTA E. KABATI Aliuliza:- Wananchi waliopisha ujenzi wa barabara ya mchepuo ya Tumaini kuchepusha magari makubwa kupita katikati ya Mji wa Iringa walilipwa fidia zao baada ya muda mrefu sana kufanyiwa tathmini. (a) Je, sheria inasemaje? (b) Je, Serikali ipo tayari kuwapatia nyongeza ya fidia zao?

Supplementary Question 1

MHE. RITTA E. KABATI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi niulize maswali madogo mawili. Kwanza nianze na kumpongeza sana Mheshimiwa Waziri kwa kazi nzuri sana ambazo wamekuwa wakizifanya. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia niipongeze sana Serikali hii ya Chama cha Mapinduzi kwa ujenzi wa mtandao wa barabara katika Mkoa wetu wa Iringa, wamefanya kazi nzuri sana. Pia kuwalipa wananchi hao fidia kwa hiyo barabara ambayo imetajwa hapo.

Katika majibu yake Mheshimiwa Waziri amekiri kwamba wananchi hao wanatakiwa walipwe fidia na riba, sasa nimuombe Waziri anijulishe. Je, ni lini? Na wanalipwa bila usumbufu kwa sababu kwa kweli kwanza walitumia karibu miaka mitano kutolipwa baada ya tathmini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, kwa kuwa changamoto ya kupitisha magari makubwa katikati ya Mji wa Iringa kumesababisha wafanyabiashara hasa wenye maduka, hoteli, migahawa kupata shida sana na wale wananchi wanaofuata huduma kwa sababu magari yao yanafungwa, kwa hiyo wanasababisha kutofanya biashara vizuri. Vilevile kumesababisha Serikali kutopata kodi ya uhakika na vilevile kuna ajali kubwa sana itakuja kutokea kwa sababu magari makubwa ya mafuta yanapita barabarani.

Je, Mheshimiwa Waziri sasa leo hii uniambie na uwaambie wananchi wa Iringa ile barabara ya mchepuo kwa sababu tumeshapata ahadi nyingi sana. Kila siku, nimeuliza kama maswali matano, lini sasa mtaijenga ili kuondoa hiyo changamoto ambayo imekuwa ni tatizo kubwa mno katika Mkoa wa Iringa? (Makofi)

Name

Eng. Isack Aloyce Kamwelwe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Katavi

Answer

WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu maswali mawili ya Mbunge Viti Maalum, Mheshimiwa Ritta Kabati kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza suala la riba ni commitment ya Serikali kwamba riba hiyo kwa wananchi italipwa baada ya fedha kutolewa kwa sababu tuko mwezi wa tisa na kwa mujibu wa sheria za kifedha, mwezi wa tisa ndiyo fedha zinaanza kutolewa. Kwa hiyo, nikuhakikishie Mheshimiwa Ritta Kabati kwamba fedha hiyo ya riba italipwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu usumbufu mwingine uliousema Serikali ilishaona, Serikali ya Chama cha Mapinduzi kwamba kuna umuhimu wa kuweka barabara ya mchepuo ili kuweza kuondoa hivyo vikwazo ambavyo mwenyewe umevitaja kwa wananchi. Kwa hiyo, nikuhakikishie, usanifu umekamilika na kama hatua tayari fidia tumeshalipa bado riba. Kwa hiyo sasa hivi taratibu za Kiserikali zinaendelea ili kuhakikisha barabara hiyo inajengwa haraka. (Makofi)