Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Richard Phillip Mbogo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nsimbo

Primary Question

MHE. RICHARD P. MBOGO Aliuliza:- Mabadiliko ya Sheria ya Fedha ya Serikali za Mitaa Sura 290 yameleta nafuu sana kwa wakulima, lakini wakati huo huo Halmashauri za Wilaya zenye wakulima zenye wakulima wadogo zimeathirika kimapato na kusababisha kushindwa kutatua kero za wananchi kwa wakati:- (a) Je, Serikali inaweza kuangalia upya suala la utoaji Ruzuku za maendeleo? (b) Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo imeathirika kiwango kikubwa: Je, Serikali ipo tayari kuipatia ruzuku ili kutoa huduma za Elimu na Afya?

Supplementary Question 1

MHE. RICHARD P. MBOGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa nafasi ili niweze kuuliza maswali madogo mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza niishukuru Serikali kwa kuangalia na kutoa ruzuku kwenye Halmashauri zetu, hususan ambazo zina vipato vya chini. Swali la kwanza; kwa kiwango hiki ambacho Serikali imetoa, bado kulingana na uhitaji kwenye Halmshauri ya Wilaya ya Nsimbo ni kidogo. Je, wako tayari kutuongezea ili tuweze kukidhi ukamilishaji wa maboma na uhitajikwenye upande wa elimu pamoja na afya?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili; katika upande wa mahitaji haya je, Naibu Waziri yupo tayari kurejea ziara yake atembelee Halmashauri ya Nsimbo kujionea na aweze kuona namna bora ya kuiwezesha Halmashauri ya Nsimbo?

Name

Mwita Mwikwabe Waitara

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tarime Vijijini

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Kwanza naomba nipokee pongezi hizi za Mheshimiwa Mbunge, na hii pia imezingatia sana kwamba amekuwa akilisemea sana eneo lake hili ili kuweza kuondoa kero.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali lake la kwanza anauliza kama Serikali ipo tayari kuongeza fedha. Naomba nimhakikishie yeye na Waheshimiwa Wabunge wote kwamba Serikali nia yake kubwa ni kuhakikisha kwamba inaondoa changamoto ya miundombinu ya elimu na afya na kazi hiyo itakuwa inaendelea kufanyika kadri ya upatikanaji wa fedha kwa Serikali na wadau mbalimbali wa maendeleo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali lake la pili ananiuliza kama nitarejea ziara katika eneo hili. Ni kweli nimeshapanga ziara karibu mara mbili ikikaribia kwenda kule eneo la Katavi na Rukwa, ziara hii imekuwa ikiahirishwa. Naomba nimhakikishie ratiba nimeshaipanga, tukiahirisha Bunge hili Mheshimiwa Mbunge nitakuja Katavi na Rukwa na ntatembelea majimbo yote ya ukanda ule. Ahsante sana.

Name

Cecil David Mwambe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ndanda

Primary Question

MHE. RICHARD P. MBOGO Aliuliza:- Mabadiliko ya Sheria ya Fedha ya Serikali za Mitaa Sura 290 yameleta nafuu sana kwa wakulima, lakini wakati huo huo Halmashauri za Wilaya zenye wakulima zenye wakulima wadogo zimeathirika kimapato na kusababisha kushindwa kutatua kero za wananchi kwa wakati:- (a) Je, Serikali inaweza kuangalia upya suala la utoaji Ruzuku za maendeleo? (b) Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo imeathirika kiwango kikubwa: Je, Serikali ipo tayari kuipatia ruzuku ili kutoa huduma za Elimu na Afya?

Supplementary Question 2

MHE. CECIL D. MWAMBE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza:

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunatambua hivi karibuni TAMISEMI wamekuwa wakitoa rating kwenye Halmashauri zetu kwa maana ya kuwapa namba kutokana na makusanyo na utekelezaji wa makusanyo wanayoyafanya. Kwa bahati mbaya sanaHalmashauri nyingi ambazo walipanga mipango yao ikitegemea makusanyo ya mazao ya kilimo hawakuweza kufanikiwa kupata hizo pesa kwa wakati kwa sababu Serikali iliamua kuingilia mchakato fulani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa nataka kuuliza kwa Mheshimiwa Waziri, kwamba miradi mingi imesimama kwenye Halmashauri zetu, pesa za posho kwa ajili ya Madiwani hazilipwi kwa wakati na hasa miradi ya afya kwa sababu hivi karibuni – na niipongeze Serikali kwamba wametupatia pesa za 4PRkwa mfano Jimbo la Ndanda tumepata zaidi ya madarasa 13. Sasa ninataka kufahamu; ni lini Serikali mtapeleka pesa kwa ajili ya kukamilisha maboma yaliyojengwa kwa nguvu za wananchi kwenye Kata za Ndanda, Lukuledi, Mihima na Mpanyani kwa ajili ya vituo vya afya?

Name

Mwita Mwikwabe Waitara

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tarime Vijijini

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana. Mheshimiwa Mwenyekiti, ameeleza maelezo mengi lakini kwa ufupi ni kwamba kama kuna mahitaji mahsusi unaandika TAMISEMI ili waweze kuyafanyia kazi. Lakini mpango wa Serikali ni kwamba hata Mwaka wa Fedha tunapoanza 2019/2020, fedha zimetengwa kwenda kumalizia maboma ambayo yapo ya msingi na sekondari katika Halmashauri zenu. Kwa hiyo tuvute subira lakini kama una jambo mahsusi tuandikie ili tuweze kuchukua hatua za haraka zaidi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini niseme hii haisemwi amesema 4PR, hii EP4R ndiyo lugha sahihi, maana yake ni kwamba Education Payment For Results. Ahsante.