Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Salum Mwinyi Rehani

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Uzini

Primary Question

MHE. SALUM MWINYI REHANI Aliuliza:- Dawa ya Sulphur ndiyo dawa ya udhibiti wa fungue (fangi) kwenye mazao ya korosho na mazao mengine, na Serikali imeunda mfumo wa kuagiza dawa hii ya kupuliza kwa njia bubu procurement; na mwaka jana baadhi ya wakulima waliathirika kwa kuchelewa na kupata dawa feki. (a) Je, ni lini Serikali itakuwa tayari kuleta dawa mbadala ambazo ni rahisi zaidi? (b) Je, ni lini Serikali itakaa na Vyama vya Msingi ili kupanga ratiba ya kuagiza na kuleta dawa na kupiga na pia kuzuia dawa za msimu uliopita?

Supplementary Question 1

MHE. SALUM MWINYI REHANI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, nauliza maswali mawili ya nyongeza; Je, Serikali ina mkakati gani wa ndani ambao utahakikisha kwamba viuatilifu vyote vinaagizwa kwa mfumo wa bulk procurement ambao sasa hivi haujaanza. Mfumo huu ndiyo ule ambao unasaidia kulifanya zao la korosho ku-stand kwenye uzalishaji mkubwa zaidi kama ulivyofanyika mwaka juzi?

Mheshimiwa Mwenyekiti, mpango wa udhibiti wa wafanyabiashara wasio waaminifu pamoja na kutumia watafiti ambao wengine wanashirikiana katika kutengeneza baadhi ya viuatilifu ambavyo wanavichanganya na dawa kama za salfa, dawa kama za pecoxystrobin na proquinazid ambazo zinachangia sana kuweza kusaidia kuongeza uwezo wa kemikali na kuua wadudu lakini vinaharibu mazingira katika maeneo yetu. Je, mkakati gani upo ambao utaweza kuwadhibiti kupitia TPRA hawa wafanya biashara ambao si waaminifu?

Name

Omary Tebweta Mgumba

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Morogoro Kusini Mashariki

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE. OMARY T. MGUMBA): Mheshimiwa Mwenyekiti, swali lake la kwanza anataka kujua mkakati wa Serikali kwa ajili ya kuanzisha mfumo wa uagizaji wa viuatilifu kwa pamoja (bulk procurement) ukoje. Nataka nimtaarifu Mheshimiwa Mbunge, Serikali sasa hivi tuko kwenye hatua za mwisho wa mchakato wa kumalizia ili kwa ajili ya uagizaji wa viuatilifu kwa pamoja. Nataka nimhakikishie msimu ujao wa kilimo cha korosho wa mwaka 2020/2021 kama nilivyojibu kwenye jibu langu la msingi, tutaagiza viuatilifu kwa pamoja kwa kutumia Mfumo wa Bulk Procurement.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali lake la pili anataka kujua mkakati wa Serikali tuliokuwa nao katika kudhibiti uingizaji nchini wa viuatilifu feki. Tulishawaelekeza Taasisi yetu ya TPRA na wako field wanafanya ukaguzi wa mara kwa mara na ukaguzi wa kushtukiza katika maduka yote ili kubaini viuatilifu ambavyo havina sifa na kuvitoa sokoni na kuchukulia hatua kwa wale walioviingiza. Pia, vyombo vyetu vya ulinzi na usalama pamoja na TRA wanadhibiti mipaka yetu kwa ajili ya kuingiza viuatilifu hivi feki ili kuwalinda wakulima hawa wapate viuatilifu vinavyostahili.