Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Eng. Joel Makanyaga Mwaka
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Chilonwa
Primary Question
MHE. JOEL M. MWAKANYAGA aliuliza:- Je, Serikali ina mpango gani wa kuitengeza barabara inayounganisha kijiji cha Bwawani kilichopo Kata ya Manchali na Kijiji cha Ikowa kilichopo Kata ya Ikowa ili iweze kupitika katika kipindi chote cha mwaka?
Supplementary Question 1
MHE. JOEL M. MWAKANYAGA: Mheshimiwa Spika, nashukuru sana kwa majibu mazuri sana ya Mheshimiwa Naibu Waziri, majibu yanayotia moyo kwa wananchi wa Jimbo la Chilonwa. Pia nishukuru kwa ujumla wake jibu limekuwa la jumla mno kwa halmashauri lakini kwa jumla mno kwa Jimbo la Chilonwa, kwamba barabara nyingi zimetengezwa mwaka jana na nyingi zimepangwa kutengezwa mwaka huu. Sasa ombi langu kwa Mheshimiwa Naibu Waziri, kwa mwaka huu wa fedha 2019/2020 ambapo zimetengwa bilioni 1.366, naiomba Serikali ifanye kila linalowezekana kuhahikisha kwamba barabara hii ya kutoka bwawani kuja Ikowa angalau inatengenezwa na angalau iwe inatengenezwa kwa zile sehemu korofi ili iweze kupitika kipindi kizima cha mwaka. Ahsante sana.
Name
Josephat Sinkamba Kandege
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kalambo
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS,TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPH S. KANDEGE): Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Makanyaga, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, kama ambavyo nimetoa majibu ya msingi kwamba uhitaji kwa ajili ya kukamilisha barabara hii ni shilingi milioni 668.2, ni kiasi kingi cha fedha na katika bajeti ambayo wametengewa ni bilioni 1.366 maana yake ukisema unamega kiasi chote barabara zingine ambazo nazo zina uhitaji maalum zitakosa kutengenezwa. Naomba Mheshimiwa Mbunge avute subra kama ambayo nimejibu kwamba Serikali inajitahidi kutafuta kiasi kingine cha fedha ili tuweze kutengeneza barabara hiyo iweze kupitika katika vipindi vyote. Katika mikoa ambayo sisi kama Taifa kipaumbele kwa barabara ni pamoja na Dodoma, ndio maana hata bajeti yake imetengwa nyingi ukilinganisha na mikoa mingine.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved