Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Christopher Kajoro Chizza
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Buyungu
Primary Question
MHE. ZUBERI M. KUCHAUKA aliuliza:- Wakati Jeshi la Polisi likitekeleza majukumu yake kumekuwa na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu na hata uvunjifu wa Katiba kwa kisingizio cha maagizo kutoka juu:- (a) Je, ni mamlaka gani iko juu ya sheria? (b) Je, maagizo hayo yanapopingwa na sheria za nchi na kukiuka haki za binadamu nini hukumu ya yule aliyetendewa kinyume cha sheria? (c) Je, huyu anayekutwa na kadhia hii hana haki ya kumjua huyo mwenye mamlaka ya juu?
Supplementary Question 1
MHE. ENG. CHRISTOPHER K. CHIZA: Mheshimiwa Spika, kwanza nashukuru kwa majibu mazuri ya Mheshimiwa Waziri nina swali moja tu la nyongeza. Kwa kuwa Mheshimiwa Kuchauka ameuliza maswali ambayo yanahusiana na utendaji kazi wa Jeshi la Polisi, na kwa kuwa yamo masuala ya ukiukwaji wa haki za binadamu. Je, Mheshimiwa Waziri uko tayari sasa ukutane na Mheshimiwa Kuchauka ili aweze kukupa maelezo kama yapo specific uweze kuyafanyia kazi?
Name
Eng. Hamad Yussuf Masauni
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kikwajuni
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI: Mheshimiwa Spika, kwanza nimpongeze kwa swali lake zuri ameuliza suala kitaalam sana na nimuahidi kwamba huo ndiyo utaratibu mzuri kwa pale ambapo wawakilishi wa wananchi kama Wabunge wanapoona kuna tatizo Specifically limejitokeza kwa wananchi wao Serikali tupo kwa sababu hiyo. Kwa hiyo, wakati wowote Mheshimiwa Kuchauka atakapokuwa amerejea tutakuwa tayari kukaa naye tuweze kujua kama anakusudia kuna tatizo mahsusi ambalo analifahamu na uthibitisho wa tatizo hilo ili tuweze kusaidiana kuchukua hatua stahiki kwa mujibu wa sheria.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved