Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Rashid Mohamed Chuachua
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Masasi Mjini
Primary Question
MHE. DKT. RASHID M. CHUACHUA aliuliza:- Mwaka 2017/2018 kulitokea mauaji ya vijana wa bodaboda katika Wilaya ya Masasi ambapo vijana wanaokaribia kuwa zaidi ya kumi wameuwawa kikatili na kunyang’anywa pikipiki:- Je, nini kauli ya Serikali kuhusu matukio haya katika Wilaya ya Masasi?
Supplementary Question 1
MHE. DKT. RASHID M. CHUACHUA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana.
Mheshimiwa Naibu Spika, swali ni la muda mrefu na majibu pia ni ya zamani, lakini hali ya mauaji ya vijana wa bodaboda katika Wilaya Masasi bado inaendelea mpaka sasa. Hata wiki tatu zilizopita tumezika vijana wawili.
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba swali la kwanza liwe Mheshimiwa Waziri atoe kauli sasa kwa kuwa Wasaidizi wake kule wameshindwa kudhibiti mauaji haya kauli yake ni ipi ili kuhakikisha kwamba vijana hawa hawapotezi maisha?
Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili; Mheshimiwa Waziri naomba atueleze ni watuhumiwa wangapi mpaka sasa wamekwishafikishwa Mahakamani kwa makosa haya?
Name
Eng. Hamad Yussuf Masauni
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kikwajuni
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Naibu Spika, kauli ya Serikali kulingana na hoja ambayo ameizungumza ni kwamba tutaendelea kuhakikisha kwamba tunadhibiti mauaji nchi nzima, hata mimi na yeye Mheshimiwa Mbunge kwa sababu anaonekana kutokuridhika na takwimu ambazo mimi naamini ni sahihi za mauaji ya watu wanne kwa mwaka 2018/2019, nitakuwa tayari tupange tuende katika Wilaya yake tuweze kuthibitisha hilo, nilifika katika Wilaya ya Masasi lakini tutakwenda tena kwa ajili ya suala hili kwa sababu suala linalogusa uhai wa Watanzania ni suala ambalo linahitajika kuchukuliwa kwa uzito unaostahiki. Kwa hiyo, ili kuweza kujua kama ana taarifa ambazo hazijafika katika Jeshi la Polisi tutazichukua na kuzifanyia kazi kwa pamoja na Jeshi la Polisi katika eneo husika.
Mheshimiwa Naibu Spika, pia kuhusiana na swali lake la kutaka kujua idadi ya watu ambao wamechukiliwa hatua, kwa wale watu wanne ambao nimewazungumza tayari watu wawili wameshakamatwa na wapo katika hatua mbalimbali za kisheria. (Makofi)
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved