Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Eng. Joel Makanyaga Mwaka
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Chilonwa
Primary Question
MHE. JOEL M. MAKANYAGA aliuliza:- Je, Serikali ina mpango gani wa kuitengeneza kwa kiwango cha kupitika muda wote wa mwaka barabara inayounganisha Kijiji cha Mbelezungu na Kijiji cha Majeleko vyote vikiwa ndani ya Kata ya Majeleko?
Supplementary Question 1
MHE. JOEL M. MAKANYAGA: Mheshimiwa Spika, ahsante. Nashukuru kwa majibu mazuri ya Serikali, lakini naomba niulize maswali mawili madogo ya nyongeza. Swali la kwanza; kutokana na vyanzo vyetu vya fedha na kutokana na mipango kazi iliyopo, je, ni lini hasa Serikali inafikiri barabara hii itafanyiwa kazi?
Mheshimiwa Spika, swali la pili; barabara hii inahusisha uwekaji wa makalavati kadhaa. Je, Serikali haioni kwamba ni vema basi kutokana na vyanzo vya fedha vilivyopo, kazi zikagawanywa katika makundi kwamba labda itengenezwe barabara kwanza na makalavati baadaye au makalavati kwanza barabara baadaye, Ahsante sana. (Makofi)
Name
Josephat Sinkamba Kandege
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kalambo
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE): Mheshimiwa Spika, katika jibu langu la msingi, nimeonesha mpaka kiasi cha fedha ambazo zinatakiwa kwa ajili ya kuhakikisha kwamba barabara hii inatengenezwa, naomba nirudie ni shilingi milioni 288.9. Tafsiri yake ni kwamba tayari tumeshabaini hata vivuko vinavyotakiwa kuwekwa na kutengeneza barabara.
Mheshimiwa Spika, pia kwa wakazi wa Dodoma na Waheshimiwa Wabunge wa Dodoma, naomba niwaondoe hofu kama kuna sehemu ambayo Serikali imeamua kuwekeza kuhakikisha kwamba miundombinu ipo ya uhakika ni pamoja na Dodoma. Hivi karibuni ukitafuta kwenye bajeti hutaiona lakini kuna jumla ya kama shilingi bilioni 84 tumeamua kuwekeza kuhakikisha kwamba ring road zinaanza kujengwa immediately.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved