Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
George Malima Lubeleje
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mpwapwa
Primary Question
MHE. GEORGE M. LUBELEJE aliuliza:- Serikali ilikuwa na Mpango wa kuifanyia matengenezo makubwa barabara ya kutoka Mima kwenda Mkanana hadi Chibwegele, Mpango huo haujatekelezwa mpaka sasa. Je, ni lini Serikali itatekeleza Mpango huo ili barabara hiyo iweze kupitika wakati wote bila matatizo kuliko ilivyo sasa?
Supplementary Question 1
MHE. GEORGE M. LUBELEJE: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi ili niulize maswali mawili ya nyongeza pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri
Mheshimiwa Naibu Spika, swali la kwanza, barabara hii ninayoizungumzia kutoka Mima – Nkanana – Chibwegele eneo korofi siyo kilomita 5 ni zaidi ya hapo. Je, Serikali ina mpango gani wa kutenga fedha za kutosha kwa sababu shilingi milioni 42 hazitoshi?
Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili nakushukuru sana Mheshimiwa Naibu Waziri kwa kutambua kwamba barabara ya kutoka Gulwe – Berege - Mima - Chitope inahitaji shilingi bilioni 1.6 ili ipate matengenezo makubwa. Sasa ni lini fedha hizi zitatafutwa ili barabara hiyo iweze kufanyiwa ukarabati? Bahati nzuri Mheshimiwa Waziri wa TAMISEMI ameshapita barabara hiyo. Ahsante.
Name
Dr. Selemani Said Jafo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kisarawe
Answer
WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza niwapongeze Naibu Mawaziri wawili kwa majibu mazuri kwa maswali ya awali.
Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Lubeleje ambaye mimi namwita greda la zamani makali yaleyale siku zote ni Mbunge ambaye anafuatilia jimbo lake, ni kweli tulipokwenda ziarani jimboni kwake tumebaini changamoto kubwa, si barabara hiyo tu hata kwenda Nambi, Tubugwe na maeneo mbalimbali kuna changamoto kubwa.
Mheshimiwa Naibu Spika, ndiyo maana ukiangalia katika bajeti ya mwaka huu na Mheshimiwa Lubeleje anafahamu kwamba kwa kuwepo na kipaumbele kwanza, sababu changamoto yake kubwa hata pale mjini tumeamua mwaka huu tutaenda kuwawekea barabara za lami lakini ile barabara ambayo ina changamoto kubwa, siku ile tulipita katika mazingira magumu sana, naomba nimwambie Mheshimiwa Mbunge kwamba awe na amani kwamba tutafanya kila liwezekanalo barabara hii ambayo kwa kweli haipitiki na shilingi milioni 42 ili kuifanya marekebisho makubwa. Hata hivyo, nimhakikishie kwamba ni commitment ya Serikali na hasa katika Jimbo la Mpwapwa na Wilaya nzima ya Mpwapwa tutafanya kila liwezekanalo ili wananchi wa Mpwapwa wafaidi matunda mazuri ya Mbunge wao ambaye ni senior MP katika Bunge hili.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved