Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Abdallah Majurah Bulembo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Nominated
Primary Question
MHE. ALHAJ ABDALLAH M. BULEMBO aliuliza:- Mnamo tarehe 20 Mei, 2019 Kampuni ya Ultimate Security iliuzwa kwa asilimia mia moja kwa kampuni ya Garda World nchini Canada. Je, Kampuni ya Garda World inatumia leseni ya kampuni ya ulinzi ya Ultimate Security au imeomba kubadili leseni ili isomeke kampuni mpya?
Supplementary Question 1
MHE. ALHAJ ABDALLAH M. BULEMBO: Mheshimiwa Spika, nina maswali mawili ya nyongeza, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, swali la kwanza, ni kanuni namba ngapi zinazoelekeza kampuni ikiuzwa asilimia mia iendelee kutumia kibali cha kampuni nyingine na jina tofauti la kampuni nyingine?
Mheshimiwa Spika, swali la pili, kwa nini brand ya Garda World itumike kama nembo badala ya kutumika kama kampuni nyingine na kwa hali hii hamuoni haki za watumishi wa kampuni ya zamani zinapotea kwa kuhalalishwa na Serikali yenyewe?
Name
Kangi Alphaxard Lugola
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mwibara
Answer
WAZIRI WA MAMBO YA NDANI NCHI: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu Maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Alhaj Abdallah Majura Bulembo, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, kwa usahihi kilichouzwa ni hisa. Hivyo wamiliki wa hisa wamebadilika lakini kampuni inabaki kama ilivyo. Hivyo Ultimate Security Company iko palepale, kwa usajili uleule na watumishi walewale na mikataba yake ileile na mali zake zote na vibali vyake vilevile na biashara yake yote. Hivyo uhalali wa kutumia vibali unapatikana na sheria iliyotumika ni Companies Act, No.12 kama ilivyorejewa 2002, Cap. 212, section 74 - 83. Hicho kinachoitwa jina lingine ni “brand name” ambalo inaruhusiwa chini ya Sheria ya Trade Marks, No.12 ya 1986, Cap.326 na Trade Mark hiyo imesajiliwa na BRELA chini ya sheria hiyo.
Mheshimiwa Spika, haki za watumishi zinabaki kama zilivyo na kilichonunuliwa ni hisa. Hivyo, kampuni na vyote vilivyomo ikiwa ni pamoja na watumishi na haki zao zinabaki kama zilivyo kwa mujibu wa mikataba yao.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved