Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Leah Jeremiah Komanya
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Meatu
Primary Question
MHE. LEAH J. KOMANYA Aliuliza: - Mji wa Mwanhuzi unakabiliwa na tatizo kubwa sana la maji safi na salama kutokana na chanzo chake cha maji cha bwawa la Mwanyahina kujaa tope: - Je, Serikali ina mkakati gani wa kuhakikisha wananchi wa Mji wa Mwanhuzi na vitongoji vyake wanapata maji safi na salama ya kutosha kwa mwaka mzima?
Supplementary Question 1
MHE. LEAH J. KOMANYA: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa majibu mazuri ya Serikali. Mradi huu ulizinduliwa mwaka 2009 na baadaye ulikabidhiwa katika Mamlaka ya Maji Mwanhuzi lakini ulipokabidhiwa usambazaji wa maji haukufanyika kama ulivyokusudiwa. Nataka kujua Serikali ina mkakati gani kuhakikisha vitongoji vya Mwambegwa, Bulianaga, Jileji na Vibiti vinasambaziwa maji ikiwemo kujengewa tanki kupitia Wakala wa Maji Vijijini?
Mheshimiwa Naibu Spika, ni dhahiri kwamba maji ya Bwawa la Mwanyahina yamefikia kiwango cha mwisho, yakitibiwa hayawezi kutakasika na wananchi tumekuwa tukiwatumainisha kuhusu ujio wa mradi wa wa maji wa Ziwa Victoria. Nataka kujua Serikali katika utekelezaji wake wa hatua za awali umefikia hatua zipi? Nashukuru. (Makofi)
Name
Maryprisca Winfred Mahundi
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Komanya, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Naibu Spika, Mradi wa Ziwa Victoria tayari utekelezaji wa awali unaendelea. Vilevile ili kuendelea kuhakikisha vijiji hivyo alivyovitaja vinaendelea kupata huduma ya maji wakati tukisubiri mradi ule wa muda mrefu tayari wataalam wetu wameweza kufanya usanifu na kuweza kuweka mkakati wa kuchimba visima 10.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa sasa tayari visima vitatu vimechimbwa na viwili angalau vimeonyesha kwamba vina maji ya kutosha. Pale Mwandoya lita 40,000 kwa saa itaweza kupatikana katika moja ya visima ambavyo vimechimbwa.
Vilevile Mwankoli kisima kimeweza kupatikana chenye uwezo wa kutoa maji lita 8,500 kwa saa. Kwa hiyo, Wizara itaendelea kuhakikisha kuona kwamba maeneo yote tunayashughulikia na maji yanapatikana bombani.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved