Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Masache Njelu Kasaka

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Lupa

Primary Question

MHE. MASACHE N. KASAKA K.n.y. MHE. ALLY A. MLAGHILA aliuliza: - Suluhisho la tatizo la maji katika Wilaya ya Kyela ni kutumia chanzo cha Ziwa Nyasa kama ilivyoelezwa kwenye Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020. Je, ni lini sasa mradi huo utaanza kutekelezwa?

Supplementary Question 1

MHE. MASACHE N. KASAKA:Mheshimiwa Spika, nashukuru sana kwa majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri, lakini kwa kuwa mpango huu wa kutumia maji ya Ziwa Nyasa ni wa muda mrefu na Serikali imekuwa inatoa ahadi hii mara kwa mara na hata kwenye ziara yako Mheshimiwa Naibu Waziri ulipofika na ulituahidi mradi huu utaanza.

Je, ni lini mradi huu utaanza ili walau kata za Kajunjumele, Ipinda, Kasumulu pamoja na Kyela Mjini waweze kunufaika?

Swali la pili kwa Wilaya yangu Wilaya ya Chunya kwa mwaka huu wa fedha zilitengwa fedha kwa ajili ya kuhudumia miradi ya maji kwa vijiji vinane lakini mpaka sasa hivi fedha hizo hazijaweza kutoka.

Je, ni lini fedha hizo zinaweza zikatoka ili sasa watu wangu wa vijiji vya Sangambi, Shoga, Kambikatoto, Lualaje, Nkung’ungu, Soweto na Itumbi waweze kunufaika nahii miradi ya maji? Nashukuru sana.

Name

Maryprisca Winfred Mahundi

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa swali la nyongeza la Mheshimiwa Ally, Mbunge wa Kyela nipende kusema kwamba upembuzi yakinifu unaendelea na muda wa kufika mwezi Mei utakamilika na tunatarajia mwaka mpya wa fedha 2021/2022 Serikali itakwenda kutekeleza mradi huo.

Kuhusiana na swali lake la nyongeza kwa Wilaya ya Chunya nipende kusema kwamba Serikali imeweka jicho la kipekee kabisa kwa Wilaya ya Chunya na Chunya ni moja ya ile miji 28 ambayo tunaitarajia kuja kuitekeleza kwa fedha ambazo tumezipata za mkopo kutoka Serikali ya India kupitia benki ya Exim. Kwa hiyo kuanzia mwezi huu Machi shughuli ya kazi katika vijiji vya Sangambi na vile vijiji vya jirani pia vinakuja kutekelezwa, ahsante.