Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Noah Lemburis Saputi Mollel
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Arumeru-Magharibi
Primary Question
MHE. NOAH L. S. MOLLEL Aliuliza:- Je, ni lini Serikali itakamilisha usambazaji wa maji kwenye Vijiji vya Engutukoiti, Losineni, Juu, Losineni kati, Oldonyawasi, Lemanda, Lemengrass, Oldonyosambu, Likurat, Olkeejulbendet, Lenigjape, Olkokula, Lemanyati, Lenjani, Seuri, Ekenywa na Ngaramtoni na Kata za Kimyak, Sambasha Tarakwa, Oloirien, Kiranyi, Likidingla, Sokon II, Olturito, Bangata, Mlanganini, Nduruma, Bwawani, Oljoro na Lahni Musa, Kisango, Mwandet Wilayani Arumeru?
Supplementary Question 1
MHE. NOAH L. S. MOLLE: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa majibu mazuri ya Naibu Waziri , lakini nina maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza; kwa kuwa Serikali ina nia njema ya kutoa huduma ya maji, kulikuwa na miradi ya mwaka 2009 miradi ya Likamba, Musa, Nengu, Olotushura na Loskito, je, ni lini sasa Serikali itakamilisha miradi hiyo ya muda mrefu?
Mheshimiwa Spika, swali langu la pili, kwa kuwa kulikuwa na ahadi ya Mheshimiwa Waziri wa Maji katika kukarabati Mradi wa Ilmuro inayohudumia Kata za Oljoro na Laroy. Je, ni lini sasa Serikali itakamilisha ahadi hiyo ya Mheshimiwa Waziri? Ahsante.
Name
Maryprisca Winfred Mahundi
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu maswali ya nyongeza ya Mheshimiwa Lemburis Saputu kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, kwa mradi huu ambao ulianza kutekelezwa mwaka 2009, nipende tu kumhakikishia Mheshimiwa Mbunge miradi hii tunakuja kuitekeleza na nimeshafika eneo lake. Nimwahidi namna ambavyo tuliongea pale site tutakuja kufanyia kazi haraka iwezekanavyo na pamoja na hii ahadi ya Mheshimiwa Waziri aliyepita, ukarabati wa Mradi huo wa Ilmuro pia unakuja kufanyiwa kazi hivi karibuni. Fedha tayari zipo na mgao unaofuata na mgao unaofuata na Mheshimiwa Mbunge yupo na atakwenda kutekelezewa mradi huo.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved