Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Mwanaisha Ng'anzi Ulenge

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. ENG. MWANAISHA N. ULENGE Aliuliza:- Miradi mikubwa ya ujenzi nchini inafanywa na kampuni kutoka Bara la Asia wakati wahandisi nchini wanasoma uhandisi kwa mitaala ya Uingereza na Marekani. (a) Je, Serikali haioni haja ya kuongeza mitaala ya Asia katika mitaala ya Vyuo vya Uhandisi ili Wahandisi wetu wapate utaalam katika miradi ya ujenzi? (b) Je, suala la kubadilishana weledi limepewa kipaumbele gani katika miradi inayoendelea kujengwa hapa nchini?

Supplementary Question 1

MHE. ENG. MWANAISHA N. ULENGE: Mheshimiwa Spika, pamoja na majibu mazuri ya Serikali, naomba kuuliza maswali mawili ya nyongeza kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, wakati mimi nilipokuwa nasoma chuo tulikuwa tunapata ziara za mafunzo (study tours) mara kwa mara kwenye maeneo ambayo kazi zilikuwa zinatendwa kwa vitendo. Hata hivyo, utaratibu huo ulikoma na tukabakiwa tu na utaratibu wa mafunzo viwandani (industrial practical training) sasa ili kuzalisha vijana mahiri, wabunifu na wenye uwezo wa kuhamisha maarifa ya kisayansi katika uzalishaji. Je, Serikali haioni haja ya kuongeza utaratibu wa study tours pamoja na huu uliopo wa mafunzo viwandani? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, swali langu la pili, niishukuru Serikali na niipongeze kwa kutambua mchango wa wataalam wanawake wa kisayansi mpaka wameamua kupanga kujenga shule za masomo ya kisayansi kila mkoa. Je, Serikali inaweka utaratibu gani sasa kuhakikisha wasichana waliofaulu vizuri masomo ya sayansi wanapata mikopo na fursa nyingine za elimu ya juu bila kuhangaika na usumbufu wowote kama ambavyo imetoa hivi karibuni?

Name

Omary Juma Kipanga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mafia

Answer

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Ulenge, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, ni kweli katika utaratibu wa kawaida vyuoni tunakuwa na program zile za practical training baada ya kumaliza mwaka husika wa masomo, lakini tumekuwa na utaratibu wa zamani ule wa kufanya study trip. Hata hivyo, kutokana na uhaba wa bajeti program hizi zilisimama.

Naomba kulithibitishia Bunge lako tukufu, hivi sasa tunakwenda kuimarisha na kuboresha bajeti yetu katika maeneo haya ya elimu, especially, katika vyuo vikuu na utaratibu huu sasa wa hizi study tour unaweza ukarejea.

Mheshimiwa Spika, katika eneo la pili ambalo ni wasichana; kama mnavyofahamu Mheshimiwa Rais wakati anahutubia Bunge hili alizungumza hapa kwamba tunakwenda kujenga shule 26 katika kila mkoa kwa lengo la kuhakikisha kwamba wasichana wanakwenda kupata study za masomo ya sayansi katika maeneo haya. Lengo la Serikali ni kuhakikisha kwamba wasichana hawa pindi watakapomaliza masomo yao haya tunakwenda kuwa-absorb kwenye vyuo ili sasa tuweze kupata wataalam wasichana na wanawake wengi katika masomo haya ya sayansi.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba kipaumbele chetu kama Serikali na katika mikopo yetu ya elimu ya juu tutahakikisha kwamba masomo haya ya sayansi yanapewa kipaumbele, hasa kwa wasichana wetu hapa nchini. Ahsante.