Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Dr. Florence George Samizi

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Muhambwe

Primary Question

MHE. DKT. FLORENCE G. SAMIZI Aliuliza: - Je, ni lini Serikali itatekeleza ahadi ya Hayati Dkt. John Magufuli, Makamu wa Rais wa sasa na Waziri Mkuu ya kujenga Kituo cha Afya Kata ya Murungu katika Wilaya ya Kibondo ili kusogeza huduma na kupunguza msongamano wa wagonjwa katika Hospitali ya Wilaya ya Kibondo?

Supplementary Question 1

MHE. DKT. FLORENCE G. SAMIZI: Mheshimiwa Spika, asante sana Mheshimiwa Waziri kwa majibu yako mazuri nichukue nafasi hii kwanza kabisa kuishukuru Serikali kwa kutupatia kituo hicho katika Kata ya Bunyambo ambayo ilikuwa hatuna kituo cha afya katika Tarafa hii ya Kibondo Mjini tangu tupate uhuru. Lakini hata hivyo Kata hii ya Murungu iko takribani kilometa 31 kutoka Kibondo Mjini ambapo kuna hospitali ya wilaya na ukizingatia kwamba sasa bado tuna kata 8 katika tarafa hii ambazo hazina kituo cha afya.

Mheshimiwa Spika, swali langu la msingi ni lini Serikali itatujengea kituo cha afya katika Kata hii ya Murungu kwa kuzingatia umbali huu?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Dkt. Florence George Samizi Mbunge wa Muhambwe kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, ninatambua na Serikali inatambua kwamba tunahitaji kupata kituo cha afya katika Kata ya Murungu na ni ahadi za viongozi wetu wa kitaifa.

Mheshimiwa Spika, nimhakikishie Serikali inaendelea kutafuta fedha na mara fedha zikipatikana tutapeleka fedha pale kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha afya, asante sana. (Makofi)