Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Flatei Gregory Massay
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mbulu Vijijini
Primary Question
MHE. FLATEI G. MASSAY K.n.y. MHE. ZAKARIA P. ISSAAY aliuliza:- Je, ni lini Wakala wa Maji Vijijini atachimba visima sita katika Vijiji vya Aicho, Gidamba, 7 Gunyoda, Silaloda, Boboa na Titiwi katika Jimbo la Mbulu Mjini?
Supplementary Question 1
MHE. FLATEI G. MASSAY: Mheshimiwa Spika, pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri, nina maswali mawili ya nyongeza.
Mheshimiwa Spika, kwa kuwa vijiji vya Aicho vina vijiji pacha vya Gembak, Kamtananat, Maretadu-Chini, Khaloda, Umburu, je, ni lini vijiji hivi vitachimbiwa visima vya maji?
Mheshimiwa Spika, swali la pili, kwakuwa Wakala wa Maji alishachimba visima sita Jimbo la Mbulu Vijijini katika Kijiji cha Khababi, Labai, Endagichani, N’ghorati, Gendaa Madadu-Juu, je, lini sasa watamalizia kazi ya usambazaji kwa sababu walishamaliza kazi ya uchimbaji? (Makofi)
Name
Maryprisca Winfred Mahundi
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu maswali ya nyongeza ya Mheshimiwa Zacharia, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, lini vijiji pacha ambavyo amevitaja Mheshimiwa Mbunge vitapata visima vya maji. Wizara tumeendelea kujipanga kwa dhati kabisa kuona kwamba kwa miezi hii miwili iliyobaki katika mwaka huu wa fedha kuna maeneo ambayo visima vitaendelea kuchimbwa na kwa mwaka ujao wa fedha tumetenga visima vingi vya kutosha karibia majimbo yote. Kwa hiyo na vijiji hivi tutaendelea pia kuvipa mgao kadri fedha tutakavyoendelea kuzipata.
Mheshimiwa Spika, kuhusu visima sita vilivyochimbwa usambazaji wa maji utaanza lini, tayari tumeendelea kujipanga, maeneo ya aina hii tunahitaji kuona wananchi wanapata maji kutoka kwenye mabomba. Kwa hiyo, usambazaji utaendelea kuwa wa haraka. Kwa eneo hili la visima sita naagiza watu wa Babati (BAWASA) wajipange vizuri kwa sababu ipo ndani ya uwezo wao waweze kukamilisha kazi hii.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved