Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Minza Simon Mjika
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. MINZA S. MJIKA aliuliza:- Je, ni lini Mradi wa Maji wa Ziwa Victoria utapelekwa katika Mkoa wa Simiyu hususani katika Wilaya ya Meatu kama inavyoelekezwa katika Ilani ya Chama cha Mapinduzi?
Supplementary Question 1
MHE. MINZA S. MJIKA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante na nashukuru sana.
Kwa niaba ya wakazi wa Wilaya ya Meatu sasa napenda niulize kwamba ni lini sasa zoezi hili litaanza kwa sababu yapata wiki mbili hivi sasa hatujapata maji katika Wilaya ya Meatu na kuna vijiji ambavyo vinaukame sana kwa mfano Bukale, Mwambegwa na Chambara ni vijiji vingi sana hatuna maji kabisa leo yapata wiki mbili wakazi wa kule tunahangaika, tunapata taabu. Serikali ituambie sasa ni lini itatuletea maji huko kwetu? Ahsante. (Makofi)
Name
Maryprisca Winfred Mahundi
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Minza Mjika kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Naibu Spika, kama jibu langu la msingi nilivyosema mwezi Agosti, 2021 mradi huu unakwenda kuanzwa na suala hili ni jana tu jopo kamili la wizara liliweza kukaa na hawa wenzetu wa KfW na Mheshimiwa Waziri aliwahitaji watoe commitment yao namna ya kuweza kutekeleza mradi huu kwa wakati.
Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Mbunge nafahamu namna ambavyo unafuatilia suala hili ninakupongeza sana. Nikutoe hofu nitaongozana na wewe tutaenda kuhakikisha kwamba kila namna ambavyo ilikuwa imepangwa inakwenda kutekelezwa kwa wakati.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved