Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Ally Juma Makoa
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kondoa Mjini
Primary Question
MHE. ALLY J. MAKOA aliuliza:- Je, ni lini Serikali itaanza kujenga Daraja la Mto Bubu ili wananchi wa upande wa pili wa mto waweze kuvuka na kupata huduma mbalimbali za kijamii?
Supplementary Question 1
MHE. ALLY J. MAKOA: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa muda wa kuuliza swali la nyongeza, nina swali moja tu. Sasa kwa sababu zoezi la ukamilishaji wa ujenzi litachukua muda mrefu kwa kuzingatia majibu ya Mheshimiwa Waziri. Sasa je, Serikali haioni haja sasa ya kujenga japo daraja la dharura kwa kupitia vyombo vyetu vya jeshi ili kunusuru kesi za vifo pamoja na upotevu wa mali za wananchi? (Makofi)
Name
Mwita Mwikwabe Waitara
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tarime Vijijini
Answer
NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la Mheshimiwa Mbunge wa Kondoa Mjini, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, kwanza naomba nimpongeze Mheshimiwa Mbunge kwa kufuatilia changamoto za wananchi wake wa Jimbo lake waliompigia kura kumleta hapa Bungeni. La pili, naomba nimwambie kwamba jambo hili tumelipokea, kabla ya kwenda kuomba vyombo vyetu vya Jeshi kuna taratibu zake, naomba nimwelekeze Katibu Mkuu Ujenzi atume mtaalam wetu katika eneo hili ili tuone kama kuna haja ya kujenga daraja la dharura kwa wakati huu na tuweze kulifanyia kazi wananchi wetu waendelee kupata huduma kama ilivyo matarajio ya Mheshimiwa Rais Mama Samia Suluhu Hassan. Ahsante.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved