Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Aloyce John Kamamba
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Buyungu
Primary Question
MHE. ALOYCE J. KAMAMBA aliuliza:- (a) Je, ni kwa nini miradi ya maji katika Mji wa Kakonko kwa muda mrefu haijakamilika? (b) Je, ni lini Mji wa Kakonko na vitongoji vyake vitapata maji safi na salama ya kutosha?
Supplementary Question 1
MHE. ALOYCE J. KAMAMBA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza maswali madogo mawili ya nyongeza.
Mheshimiwa Spika, katika majibu ambayo ameyatoa ametaja mradi wa maji katika Kijiji cha Muhange ambao unapata maji kutoka Mto Mgendezi kwenda Muhange Centre na kwenda Muhange ya Juu. Hata hivyo mradi huu sasa maji yanayotoka hayafai kwa matumizi ya binadamu kwasababu ni machafu. Lakini vilevile mradi huu haukukamilika kama ilivyokusudiwa. Je, nini kauli ya Serikali kuhusiana na mradi huu?
Pili, kutokana na mradi wa maji na changamoto hizi ambazo nimezitaja, Mheshimiwa Waziri yuko tayari kufuatana nami ili akazione hizo changamoto na hatimaye kutoa suluhu ya miradi hii?
Name
Julius Kalanga Laizer
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Monduli
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa niaba ya Waziri wa Maji naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Aloyce Kamamba kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, nipende kusema nimesikitika kuona kwamba Mheshimiwa Mbunge anasema maji ni machafu na mradi haujakamilika vizuri kwa sababu swali lake la pili ni ombi la kuambatana na mimi nipende kukuhakikishia Mheshimiwa Mbunge mara baada ya Bunge hili tutakwenda pamoja na nitakwenda kujihakikishia na wakati tunaendelea kukamilisha session hii ya Bunge ninatoa maagizo kwa Meneja wa eneo lile aweze kuwajibika haya maji yaweze kufanyiwa treatment kadri ya utaalamu wetu wa Wizara ili wananchi waweze kupata maji safi na salama. (Makofi)
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved