Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Issa Ally Mchungahela
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Lulindi
Primary Question
MHE. ISSA A. MCHUNGAHELA aliuliza:- (a) Je, ni lini Serikali itawalipa wananchi wanaodai miche ya mikorosho deni ambalo ni la muda mrefu tangu mwaka 2017?
Supplementary Question 1
MHE. ISSA A. MCHUNGAHELA: Mheshimiwa Spika, nimekuwa nikifuatilia suala hili kwa muda mrefu sana na majibu yamekuwa ni hivihivi. Naomba Serikali itoe commitment ni lini watalipa deni hili.
Mheshimiwa Spika, kumekuwa na kutokuwa na umakini hasa hasa katika ulipaji wa madeni ya ndani, Serikali haioni sasa ni muda wa kulipa riba katika madeni haya ya ndani pia kama vile wanavyolipa madeni ya nje na riba.
Name
Hussein Mohamed Bashe
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Nzega Mjini
Answer
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, naomba kumjibu Mheshimiwa Mchungahela maswali yake mawili ya nyongeza kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, suala la riba, mikataba ilikuwa haionyeshi kwamba kutakuwa na riba pale ambapo kunapokuwa kuna ucheleweshaji lakini siwezi kutoa commitment ya hilo jambo.
Mheshimiwa Spika, kuhusu lini watalipwa nataka nimuhakikishie tu Mheshimiwa Mbunge na kweli amekuwa akifuatilia yeye na Wabunge wa Mkoa wa Lindi na Mtwara na baadhi ya maeneo mengine ya nchi yetu kuhusu hawa waliogawa miche. Niwahakikishie kwamba mwaka ujao wa fedha watalipwa watu wote waliosambaza miche na sisi Wizara ya Kilimo tumeshamaliza zoezi hili na tumepeleka hazina.
Mheshimiwa Spka, vilevile waliokuwa watumishi wa umma kwa maana ya Wakurugenzi na Madiwani kwa kuwa kulikuwa na mikataba halali, haki zao zitalipwa na haziwezi kudhulumiwa kwa kuwa tu ni mtumishi wa umma. (Makofi)
Name
Cecil David Mwambe
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ndanda
Primary Question
MHE. ISSA A. MCHUNGAHELA aliuliza:- (a) Je, ni lini Serikali itawalipa wananchi wanaodai miche ya mikorosho deni ambalo ni la muda mrefu tangu mwaka 2017?
Supplementary Question 2
MHE. CECIL D. MWAMBE: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Kama ilivyo madeni kwa wakulima waliozalisha miche ambao hawajalipwa lakini Serikali inakiri kuwatambua. Pia kuna watu waliotoa huduma mbalimbali kwenye msimu ule wa korosho ambao Serikali ilinunua; watu walisambaza magunia, vifungashio na wengine sulphur. Tunataka pia Serikali itoe commitment kwa sababu watu hao walikopa kwenye mabenki, ni lini nao mtamalizana nao kwa kuwalipa pesa zao. (Makofi)
Name
Hussein Mohamed Bashe
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Nzega Mjini
Answer
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Cecil Mwambe. Ni kweli kwamba katika sekta ya korosho sio tu madeni yaliyotokana na msimu ambao Serikali ilinunua korosho a wakulima. Madeni yaliyotokana na Serikali/korosho zilizochukuliwa na wakulima, Serikali imelipa sehemu kubwa na imebaki kiwango kidogo kisichozidi shilingi bilioni 2.8 ambazo zimahusisha madeni ya wasambazaji wa watoa huduma lakini sekta nzima ya korosho kuanzia vyama vya msingi, Vyama Vikuu vya Ushirika, wakulima wenyewe wanadaiwa zaidi ya bilioni 66.
Mheshimiwa Spika, kama Serikali hatua tuliyoichukua ya kwanza ni kukaa na wadai wote ikiwemo mabenki na watoa huduma na tukaweka utaratibu ambao tumeanza ku-collect fedha ambazo tutaanza kulipa kwa wale wanaohakikiwa na mchakato huo umekwishaanza na utaratibu unaendelea na kwa kuwa tutakuwa na kikao tarehe 6 Lindi ambacho kitaongozwa na Waziri Mkuu, naamini kwamba yote haya tutayajadili na tutatoka na majibu na wadai wote tumewaalika katika mkutano huo.
Name
Mussa Azzan Zungu
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ilala
Primary Question
MHE. ISSA A. MCHUNGAHELA aliuliza:- (a) Je, ni lini Serikali itawalipa wananchi wanaodai miche ya mikorosho deni ambalo ni la muda mrefu tangu mwaka 2017?
Supplementary Question 3
MHE. MUSSA A. ZUNGU: Mheshimiwa Spika, nikushukuru sana. Vietnam mwaka 1993 ilikuwa ni nchi maskini sana na walikuwa wanapewa msaada wa chakula. Leo Vietnam wanazalisha surplus ya mpunga tani milioni 20 na hii ilitokana na geographical diversification policy kwenye kilimo. Wame- map nchi yao na ile sera wakaiweka, haikuwa ni sera blanket moja ya nchi nzima, kila mapping ya eneo wakafanya diversification wa kujua eneo gani litumie sera ipi.
Mhesimiwa Spika, je, leo Serikali yetu ina mkakati gani wa kuhakikisha kuongeza tija ya kilimo na kuipitia upya sera ya kilimo nchini? (Makofi)
Name
Hussein Mohamed Bashe
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Nzega Mjini
Answer
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali alilouliza Mheshimiwa Zungu, Mbunge wa Ilala kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, ni kweli kwa muda mrefu tumekuwa kama Taifa tukifanya makosa makubwa kufikiria kwamba kilimo kila zao linaweza likalimwa kila sehemu tuka- think of extensive instead ya intensive agriculture. Kwa hiyo, mkitazama hata bajeti ya mwelekeo wa Wizara ya Kilimo tumeangalia zaidi kuhangaika namna gani tunaongeza tija. Mwelekeo wa bajeti yetu katika mwaka ujao wa fedha ume- focus katika tija badala ya kufikiria kuongeza kila zao kila sehemu.
Mheshimiwa Spika, hivi karibuni tunaomba ofisi za mamlaka ya juu, tutazindua timu mbili ambayo mojawapo ni suala la financing na nyingine ni suala la kupitia upya Sera na mtazamo wetu wa kilimo na tunaamini kwamba baada ya hapo tutakuwa na roadmap ambayo inaonyesha kila eneo litakuwa na specialty yake kutokana na competitive age yake na huko ndipo tutakapowekeza zaidi na teknolojia za kisasa katika hayo maeneo badala ya kufikiria kila zao linaweza kulimwa kila sehemu katika nchi. Kwa hiyo, huo ni mwelekeo wa Wizara na huko ndipo tunapotaka kwenda kama nchi.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved