Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Jacquline Andrew Kainja
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. JACQUELINE K. ANDREA aliuliza:- (a) Je, Serikali ina mpango wa kuwajengea miundombinu ya kisasa akina mama wa Tabora itakayoweza kukausha mboga kama uyoga, mchicha na majani ya maboga kwa njia ya kisasa zaidi ili kuongeza kipato? (b) Je, Serikali ina mpango gani wa kuboresha masoko ya ndani na nje ya nchi ilia kina mama wa Tabora wanaokausha mboga waweze kuuza mboga hizo kwa faida?
Supplementary Question 1
MHE. JACQUELINE K. ANDREA: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipatia nafasi ya swali la nyongeza. Kutokana na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri yanayowapa matumaini wafanyabiashara wa usindikaji wa mbogamboga hasa kwa Mkoa wa Tabora hususan kinamama.
Je, ni lini Serikali kushirikiana na FAO inaweza kuanza mradi huu wa kuwawezesha kina mama kuweza kufanya biashara ya Kitaifa na Kimataifa?
Mheshimiwa Spika, je, Serikali ina mkakati gani wa makusudi kuwezesha mazao haya ya usindikaji wa mbogamboga ambayo wakinamama wengi wa Mkoa wa Tabora wamejikita katika biashara hiyo kuhakikisha kwamba yanakuwa yana masoko ndani ya nchi na ukizingatia unaweza ukaenda kwenye hoteli nyingi hatuna mboga za asili, tunatumia mboga ambazo ni roast na zilizoungwa ungwa zaidi. Naomba kupata jibu, ahsante sana. (Makofi)
Name
Hussein Mohamed Bashe
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Nzega Mjini
Answer
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, naoba kumjibu Mheshimiwa Jacqueline maswali yake ya nyongeza kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, lini tunaanza mradi wa FAO, tunaaza mwaka wa fedha unaokuja; ni mradi wa miaka mitano, tunaanzia majaribio katika Wilaya ya Kaliua ndipo tutakapoanzia. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, kuhusu suala la kuwasaidia wakinamama wa Mkoa wa Tabora na Watanzania wote kuweza kuingia katika masoko. Sasa hivi tunapata project pamoja na wenzetu wa SIDO ili waweze kukidhi vigezo vya viwango vinavyoweza kuwasaidia kuingia katika masoko ndio maana mmesikia katika Mkoa wa Tabora tumesema kwamba Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na Umoja wa Wanyabiashara sasa hivi pamoja na SIDO inatafutwa eneo moja ambalo litakuwa ni center ya kina mama kwa ajili ya kukaushia na hapo kuweza kufanya packaging waweze ku- meet standard za masoko. Kwa hiyo, ni hatua ambazo zinachukuliwa na Serikali.
Mheshimiwa Spika, jambo la msingi sio tu kuzalisha, je tunachokizalisha kinaweza kukidhi vigezo vinavyotakiwa vya sokoni, hiyo ndio kazi tunayoifanya katika sekta ya mbogamboga na matunda.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved