Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Silvestry Fransis Koka
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kibaha Mjini
Primary Question
MHE. SILVESTRY F. KOKA aliuliza:- Jimbo la Kibaha Mjini bado lina changamoto kubwa ya maji katika maeneo ya Kata za Mbwawa na Pangani; na Mradi wa Ujenzi wa matanki ya maji unakwenda kwa kusuasua. Je, ni lini Mradi huo utakamilika ili Wananchi wa Kibaha Mjini waondokane na adha ya maji?
Supplementary Question 1
MHE. SILVESTRY F. KOKA: Mheshimiwa Spika, asante. naipongeza Serikali kupitia DAWASA kwa kazi nzuri iliyofanyika kule Mbwawa wananchi sasa wamepata maji kwa mradi kukamilika kwa asilimia 90. Pamoja na hayo nina maswali mawili madogo ya nyongeza:-
Mheshimiwa Spika, mradi huu wa matenki mawili ya maji katika Kata ya Pangani, kwa maana ya Mtaa wa Vikawe na Mtaa wa Pangani, unaodhaminiwa na Benki ya Dunia unajengwa kwa kusuasua. Tenki la Vikawe limefikia asilimia 50, lakini tenki la Pangani kwa ajili ya kuhakikisha sasa wananchi wa Kata ya Pangani wote wanapata maji bado halijaanza kujengwa. Je, Serikali ina mpango gani wa kuhimiza sasa, ili hili tenki la pili liweze kuanza kujengwa?
Mheshimiwa Spika, lakini swali la pili, wananchi wa Kata ya Misugusugu na Visiga na hususan maeneo ya Zogoale, Jonuga pamoja na Saeni, kupitia Zegereni Viwandani, wana shida kubwa ya maji na wanahangaika kutumia maji ya visima na haya ni maeneo muhimu ya uchumi katika Jimbo letu la Kibaha Mjini. Ninafahamu kuna mradi wa takribani bilioni 3.3 unaotakiwa kujengwa.
Je, ni lini Serikali sasa inaanza kujenga mradu huu, ili kuwaondolea wananchi kero na kustawisha uchumi katika Mji wetu wa Kibaha?
Name
Maryprisca Winfred Mahundi
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Silvestry Koka, Mbunge wa Kibaha Mjini, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, Mji wa Kibaha ni moja ya miji ambayo Serikali imeelekeza fedha nyingi kwa kuona kwamba, maji sasa yanakwenda kupatikana. Katika eneo la Pangani ni mradi mkubwa ambao tayari Serikali mpango ni kuelekeza zaidi ya bilioni tano na kazi zinatarajiwa kuanza mapema robo ya kwanza ya mwaka wa fedha ujao, kwa maana ya kuanzia mwezi wa tisa tunatarajia kazi itaenda kuanza katika mradi huu.
Mheshimiwa Spika, lakini vilevile katika maeneo ya viwandani, kama mwenyewe Mheshimiwa Mbunge alivyoongea, na nipende tu kumshukuru kwa kuweza kutoa pongezi zake kwa Serikali. Ni kweli Wizara bado imelekeza fedha za kutosha zaidi ya bilioni tatu na katika mwaka ujao wa fedha tunatarajia mradi huu uweze kutekelezwa na kasi ya mradi huu itategemea upatikanaji wa fedha katika Wizara, lakini lengo letu kubwa tunaelekea kwenye mageuzi makubwa. Miradi kama hii yote mikubwa tutahakikisha tunaisimamia kwa wakati.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved