Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Sagini Jumanne Abdallah
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Butiama
Primary Question
MHE. JUMANNE A. SAGINI aliuliza: - Je, lini Serikali itaanza rasmi ujenzi wa Chuo Kikuu cha Mwalimu Julius K. Nyerere cha Teknolojia na Kilimo, Butiama?
Supplementary Question 1
MHE. JUMANNE A. SAGINI Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa majibu mazuri ya Serikali, kwa kweli yanaleta matumaini. Hofu yangu ni moja tu, kwamba hizi lugha za mchakato, mchakato wakati mwingine unaweza ikachukua muda mrefu. Wakati nachangia hotuba ya bajeti ya Wizara hii, waliniahidi kwamba mwaka wa fedha utakapoanza utaanza harakati za ujenzi. Lakini hadi leo wanazungumzia mchakato, sasa hebu atuhakikishie hii michakato ya ku- procure huyo consultant ili afanye review ya hizi design zitakamilika lini na ujenzi uweze kuanza? Ahsante.
Name
Omary Juma Kipanga
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mafia
Answer
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Jumanne Abdallah Sagini, Mbunge wa Butiama kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika kama nilivyoeleza kwenye jawabu la msingi kwamba taratibu zote sasa zimekamilika; na upatikanaji huu wa fedha kama nilivyozungumza kwamba umeanza mwezi wa Septemba. Tunatarajia kama mambo yote yatakwenda vizuri mpaka kufika mwezi wa Februari shughuli za ujenzi katika eneo hili inawezekana zikawa zimeanza rasmi. Ahsante sana.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved