Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Nicholaus George Ngassa
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Igunga
Primary Question
MHE. NICHOLAUS G. NGASSA aliuliza: - Je, ni lini Serikali itaipandisha hadhi barabara ya Igurubi – Mbutu – Igunga hadi Itumba yenye zaidi ya km 140 kuwa chini ya TANROADS ili ijengwe kwa kiwango cha lami?
Supplementary Question 1
MHE. NICHOLAUS G. NGASSA: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kumwambia Naibu Waziri kwamba tulishapeleka maombi na Serikali ilituma wataalam wakafanya survey mwaka 2013/2014, lakini pia na mwaka 2016 walikuja wakafanya survey wakawa wamewasilisha Wizarani.
Mheshimiwa Spika, ukiangalia barabara hii ndiyo kiunganishi cha Mkoa wa Tabora na Mkoa wa Simiyu ambao kimamlaka ulitengenezwa mwaka 2012.
Kwa hiyo, namwomba Waziri aweze kulipa kipaumbele, walifikirie ombi letu na waweze kuipandishwa hadhi ijengwe kwa kiwango cha lami. Ahsante. (Makofi)
Name
Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ileje
Answer
NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE): Mheshimiwa Spika, napenda kupokea ushauri wa Mheshimiwa Nicholaus George Ngassa, kama alivyoomba.
Mheshimiwa Spika, naomba nimhakikishie kwamba kama limeshafika Wizarani, basi tutaliangalia tuone kama limekwama; na kama kuna vigezo ambavyo vinashindikana, basi nitaomba tuwasiliane naye ili kama kuna shida tuone. Kama inakidhi vigezo vyote, nadhani barabara hii itapandishwa hadhi. Ahsante.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved