Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Bupe Nelson Mwakang'ata

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. BUPE N. MWAKANG’ATA aliuliza: - Je, ni lini Serikali itakamilisha ujenzi wa barabara ya kutoka Kalambo Falls hadi barabara kuu inayokwenda Matai yenye urefu wa kilometa17?

Supplementary Question 1

MHE. BUPE N. MWAKANG’ATA: Mheshimiwa Spika, ahsante nashukuru sana, kwanza naipongeza Serikali kwa kazi inayoondelea, lakini pia nina swali moja la nyongeza.

Mheshimiwa Spika, kwa kuwa maporomoko haya ya Kalambo Falls ni kivutio kikubwa sana kwa Mkoa wa Rukwa, sasa Serikali ina mpango gani wa kujenga lami kwa sababu wawekezaji na watalii wanapenda sana vitu vizuri kama lami, vitu vizuri kama umeme. Sasa Serikali ina mpango gani wa kutengeneza miundombinu kwenye maporomoko hayo? Ahsante. (Makofi)

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DAVID E. SILINDE): Mheshimiwa Spika, ahsante sana, naomba kujibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Bupe Nelson Mwakang’ata Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Rukwa, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, niseme tu kwamba hili alilolileta Mheshimiwa Mbunge ni ombi kwa sababu ya umuhimu mkubwa wa maeneo haya ya maporomoko ya Kalambo Falls. Kwa hiyo na sisi tuseme tu kwamba tumelipokea tutafanya tathimini na tutaangalia mfuko wetu jinsi ulivyo kama fedha itapatikana basi tutailekeza Ofisi ya Rais kupitia TARURA Kalambo waweze kwenda kujenga huko. Lakini kwa sasa tutakwenda kufanya tathimini halafu tuone jinsi tutakavyopata fedha kwa ajili ya ujenzi wa lami katika eneo hilo. Ahsante sana.