Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Luhaga Joelson Mpina
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kisesa
Primary Question
MHE. LUHAGA J. MPINA K.n.y. MHE. ESTHER L. MIDIMU aliuliza: - Mwaka 2018 Mkoa wa Simiyu ulitenga eneo kwa ajili ya ujenzi wa Kiwanda cha Kuzalisha Vifaa Tiba vitokanavyo na malighafi ya pamba na utaratibu wa kuanza ujenzi umeshakamilika, lakini kibali cha ujenzi toka Serikali kuu kimechukua muda mrefu. Je, ni lini Serikali itatoa kibali kuruhusu ujenzi kuanza?
Supplementary Question 1
MHE. LUHAGA J. MPINA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nasikitika sana kwa majibu haya yaliyotolewa na Serikali. Kipindi cha miaka minne toka mwaka 2018 mpaka leo Serikali inazungumzia suala la tathmini, inazungumzia suala la upembuzi yakinifu, miaka minne! Wananchi wa Simiyu wamechoka na hizi danadana za Serikali, leo tunataka tuambiwe nini sababu zilizozuia mradi huu kujengwa ili tujue, kwa sababu huwezi kutuambia hadi miaka minne unazungumzia tathmini, unazungumzia upembuzi yakinifu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili, ni nchi yetu imekuwa ikiagiza bidhaa za nguo kutoka nje ya nchi kutokana na ukosefu wa viwanda kama hivi, tunaagiza bidhaa za nguo kutoka nje tunatumia fedha nyingi za kigeni kuagiza bidhaa za nguo nje ya nchi. Lakini pia wananchi wa Tanzania wanateseka kwa kukosa soko zuri la pamba kwa sababu ndani ya nchi hakuna viwanda na kugeuka kuwa soko la wakulima wa nchi zingine kwa kununua bidhaa zao.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sababu ajira zetu tunazi-export kila leo; Serikali ituambie ni lini Serikali itachukizwa na mambo haya na kuingia kwenye uwekezaji wa viwanda vya pamba ili wakulima wa pamba waweze kupata bei nzuri na tuweze kunufaika na valua addition la zao la pamba? (Makofi)
Name
Dr. Godwin Oloyce Mollel
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Siha
Answer
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nimpongeze Mbunge kwa swali lake zuri la nyongeza na ni kweli akisikitika ana haki ya kusikitika, lakini kiukweli ilikuwa ni lazima taasisi yetu ya TIRDO ifanye upembuzi yakinifu wa kuhakikisha kwamba kinachokwenda kufanyika je, kinaweza kuleta manufaa tarajiwa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini vilevile ikumbukwe kwamba kuna mifuko kama mitano ambayo ilikuwa ichangie kwenye ujenzi huo; kwa maana ilikuwa kwanza ni kuhakikisha hii mifuko inakubaliana na module operant pamoja na kufanya hayo mambo mengine, lakini kimsingi ilionekana vilevile katika upembuzi yakinifu ndiyo maana utaona upembuzi wa kwanza ulionesha tunahitaji shilingi bilioni 59.4 kujenga. Lakini wakati wakifanya mchakato wakaona kwamba kuna uwezekano wa kuokoa hizo shilingi bilioni 51.
Sasa labda Mheshimiwa anasema ni lini tutamalizana na jambo hilo, labda Mheshimiwa Mbunge nikuombe kitu kimoja kabla ya tarehe 15 Machi, 2022 tayari kitaitishwa kile kikao ambacho kitaelezea muafaka wa hili jambo na Mheshimiwa Mbunge tutawaalika Wabunge wa Mkoa wa Simiyu ili tuweze kukubaliana way forward kwa pamoja.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved