Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Haji Amour Haji
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Makunduchi
Primary Question
MHE. HAJI AMOUR HAJI aliuliza: - Je, Serikali haioni haja ya kuwa na Chombo Maalum (Agency) kitakachosimamia shughuli zote za kampuni binafsi za ulinzi ili kuongeza wigo wa kiutendaji pamoja na kuwepo kwa sheria itakayosimamia kampuni hizo?
Supplementary Question 1
MHE. HAJI AMOUR HAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Kwa vile Serikali inatambua umuhimu wa kuwepo kwa sheria ya makampuni ya ulinzi binafsi, swali langu ni hili; je, sheria gani kwa sasa hivi inayotumika kuwapatia vibali hayo makampuni binafsi ya ulinzi?
Mheshimiwa Spika, ahsante.
Name
Sagini Jumanne Abdallah
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Butiama
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Kwa sasa hakuna sheria mahususi kwa ajili ya kazi hiyo, badala yake inatumiwa miongozo inayotolewa na Mkuu wa Polisi Nchini (IGP).
Name
Amina Daud Hassan
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. HAJI AMOUR HAJI aliuliza: - Je, Serikali haioni haja ya kuwa na Chombo Maalum (Agency) kitakachosimamia shughuli zote za kampuni binafsi za ulinzi ili kuongeza wigo wa kiutendaji pamoja na kuwepo kwa sheria itakayosimamia kampuni hizo?
Supplementary Question 2
MHE. AMINA DAUD HASSAN: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa kunipa nafasi hii. Kwa kuwa tunayo makampuni mengi ya binafsi katika nchi yetu: -
Je, ni lini Serikali italeta Muswada wa kuwa na Sheria ya Makampuni Binafsi ya ulinzi? (Makofi)
Name
Sagini Jumanne Abdallah
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Butiama
Answer
NAIBU WAZIRI, WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Spika, kama nilivyojibu kwenye swali langu la msingi ni kwamba mashauriano yanaendelea baina ya Serikali zetu mbili; Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ili turidhiane. Kwa sababu suala hili linagusa Muungano, hatuwezi kulifanya upande mmoja wa Muungano tukasema tumekamilisha.
Mara taratibu hizo zitakapokamilika, then tutapeleka Muswada kwa ajili ya kupitiwa na kuridhiwa na Bunge.
Mheshimiwa Spika, nashukuru. (Makofi)
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved