Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Norah Waziri Mzeru
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. NORAH W. MZERU aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kuufanya Mkoa wa Morogoro kuwa moja ya kitovu kikuu cha utalii duniani kwa kuwa ni Mkoa wenye vyanzo vingi vya utalii?
Supplementary Question 1
MHE. NORAH W. MZERU: Mheshimiwa Spika, ahsante sana, pamoja na majibu mazuri ya Serikali, je, kuna mpango gani wa kuwavutia wawekezaji katika sekta ya utalii Morogoro? (Makofi)
Name
Mary Francis Masanja
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Spika, ahsante, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Norah Mzeru, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, awali ya yote nimpongeze sana Mheshimiwa Norah kwa kuendelea kuimarisha utalii, lakini pia kuendelea kuhamasisha katika maeneo mbalimbali ikiwemo maeneo yaliyohifadhiwa katika Mkoa wa Morogoro.
Mheshimiwa Spika, nipende tu kumtaarifu Mheshimiwa Mbunge kwamba Serikali imeweza kuainisha maeneo mbalimbali kwenye maeneo yaliyohifadhiwa kwa ajili ya kuwekeza na shughuli hizi za uwekezaji zinahamasishwa katika maeneo mengine mengi ambayo utalii unafanyika. Hivyo, nimtoe wasiwasi katika hifadhi ya Udzungwa, Mikumi, pamoja na Nyerere, tumetenga maeneo mahususi kwa ajili ya uwekezaji. Hivyo, tunaendelea kuwaalika wawekezaji wa ndani ya nchi na nje ya nchi waweze kufika katika maeneo hayo na kuwekeza kwa ajili ya kuongeza na kukuza utalii. Ahsante.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved