Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Anthony Calist Komu

Sex

Male

Party

CHADEMA

Constituent

Moshi Vijijini

Primary Question

MHE. ANTONY C. KOMU (K.n.y. MHE. HAWA S. MWAIFUNGA) aliuliza:- Kumekuwa na ukiukwaji mkubwa wa maadili ya utumishi ndani ya Jeshi la Polisi kutokana na hilo Askari wengi wanaonekana kukosa weledi kwa kujihusisha na matendo yanayokinzana na maadili ya utumishi wa umma:- (a) Je, Serikali inachukua hatua gani kuhakikisha kuwa Askari wasio na sifa wanachukuliwa hatua? (b) Je, zoezi la kuhakiki vyeti vya Askari wasio na sifa ndani ya Jeshi la Polisi limefikia wapi?

Supplementary Question 1

MHE. ANTONY C. KOMU: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa majibu ya Mheshimiwa Naibu Waziri isipokuwa kwa mujibu wa Tume mbalimbali za Haki za Binadamu na hasa ile ya Umoja wa Mataifa ratio ya polisi na wananchi wanasema inapaswa kuwa 1:450 lakini katika nchi yetu ni 1:1300. Mheshimiwa Waziri amesema kwamba wameamua kusitisha kwa muda ajira kutokana na mambo hayo mengine ambayo wanayafanya, naomba niulize haoni kwamba kufanya hivyo ni kuendelea kukuza lile tatizo la uwiano? Pia katika hiyo ratio ambayo nimeitaja, wanawake ni wachache kweli na ndiyo maana hata humu ndani ya Bunge ikitokea kitu chochote askari wa kiume wanakuja kuwakabili wanawake kwa sababu ya upungufu. Hilo ni swali la kwanza. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, zipo taarifa kwamba katika jeshi letu wako watu wanaajiriwa na inachukua muda sana kwenda kwenye mafunzo ya msingi ya uaskari wakati jambo hili la uaskari linahitaji maadili ambayo ni maalum kwa sababu ni jambo nyeti. Siku zote kisingizio kimekuwa ni bajeti, sasa nataka kujua hali ikoje sasa hivi kama wameshakuwa na uwezo wa kumudu hali hiyo? Ahsante.

Name

Eng. Hamad Yussuf Masauni

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kikwajuni

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Naibu Spika, nirekebishe kidogo, uwiano wa askari kimataifa ni askari 1:400 na kwa upande wa Tanzania Bara ni askari 1:1200, kwa hiyo kidogo kuna utofauti na maelezo ambayo ametoa Mheshimiwa Mbunge. Niseme tu usitishaji huu hauathiri kwa sababu ni usitishaji wa muda mfupi sana, kuna mambo tu kidogo ambayo yanawekwa sawa, nadhani muda si mrefu tutaendelea na utaratibu wetu kama kawaida.
Mheshimiwa Naibu Spika, lakini kuhusiana na swali lake la pili kwamba kuna upungufu wa wanawake katika Jeshi la Polisi, ni kweli na tunapoelekea kwenye fifty-fifty basi nitoe wito tu kwa wanawake kuhamasika zaidi ili kujiunga na vyombo vya ulinzi na usalama.