Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Abeid Ighondo Ramadhani
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Singida Kaskazini
Primary Question
MHE. ABEID R. IGHONDO aliuliza: - Wananchi wa Kata za Mgori, Mughungu na Ngimu Jimbo la Singida Kaskazini wapo tayari kukabidhi Msitu wa Mgori kwa Serikali kuwa Hifadhi ya Taifa: - Je, mchakato wa Serikali kukamilisha zoezi hilo umefikia wapi na faida gani wananchi watazipata kwa msitu huu kuwa hifadhi?
Supplementary Question 1
MHE. ABEID R. IGHONDO: Mheshimiwa Spika, nakushukuru, pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri, nitoe pia shukrani zangu za dhati kwa hatua hiyo iliyofikiwa ambapo sasa wanyama kama vile tembo, twiga, swala na wengineo wameongezeka sana. Sasa naomba kuliza maswali mawili madogo ya nyongeza.
Mheshimiwa Spika, swali la kwanza, je ni kwa namna gani sasa wananchi wanaozunguka msitu ule wameshirikishwa ikiwa ni pamoja na kupewa elimu ili kuepusha migogoro na migongano isiyokuwa na lazima inayoweza kujitokeza? (Makofi)
Mheshimiwa Spika, lakini pili, je, Serikali inatoa commitment gani wakati wa kutoa tangazo sasa la kuumiliki ule msitu, kupeleka mizinga ili wananchi waone fursa yaani wanufaike na zile fursa zinazotokana na huo msitu ili nao wawe sehemu ya kuutunza huu msitu? Naomba kuwasilisha. (Makofi)
Name
Mary Francis Masanja
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Spika, ahsante, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Abeid Ramadhani, Mbunge wa Singida Kaskazini kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, kama nilivyojibu kwenye majibu yangu ya msingi ni kwamba Serikali tumeendelea kupongeza Serikali za Vijiji, Wilaya na Mikoa kwa hatua ambayo wamefikia kwamba maamuzi waliyoyafanya kwanza ni mazuri; lakini pia nimuondoe wasiwasi Mheshimiwa Mbunge kwamba tutakapokuwa tumeshakamilisha tangazo na kuwa na GN ya eneo lile basi tutaanza kuelimisha wananchi wanaozunguka maeneo hayo kuangalia na kuona faida za kuhifadhi huo msitu. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, lakini pia faida nyingine zinazopatikana katika maeneo hayo ikiwemo kuhamasisha wananchi kujiendeleza na faida ya ufugaji nyuki ili kuweza kupata zao la asali lakini kwa wakati huo huo tunaweza tukaendelea kutangaza utalii na likawa eneo mojawapo la kuhamasisha watu kwenda kutembelea katika maeneo hayo. (Makofi)
Mheshimiwa Spika hizi zote ni faida kwa wananchi na watarajie kwamba watafaida nae neo hili kwa sababu uhifadhi ni moja ya maeneo ambayo tunaendelea kuhamasisha nchini kote. Ahsante. (Makofi)
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved