Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Francis Leonard Mtega
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mbarali
Primary Question
MHE. FRANCIS L. MTEGA aliuliza: - Je, kuna mpango gani wa kuboresha Hifadhi ya Taifa Kitulo?
Supplementary Question 1
MHE. FRANCIS L. MTEGA: Mheshimiwa Spika, nakushuruku sana lakini pia nashukuru sana majibu mazuri ya Serikali, hata hivyo, nina maswali mawili madogo ya nyongeza.
Kwanza, kutoka barabara kuu kufika Kitulo pana mlima wenye kona 54 na nyani wa kutosha. Je, Serikali ina mpango gani wa kutengeneza barabara ile kwa kiwango cha lami ili watalii wakafurahie nature ya uumbaji wa Mwenyezi Mungu? (Makofi)
Mheshimiwa Spika, pili; je, Wizara ina mpango gani wa kujenga ofisi walau ndogo pale Chimala ili kuamsha ari ya wananchi pale kujenga mahoteli ya kitalii jambo ambalo litaleta fursa ya ajira kwa vijana na kuinua uchumi wa Wanambarali? (Makofi)
Name
Mary Francis Masanja
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Francis Leonard Mtega, Mbunge wa Mbalali kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, ni kweli kuna changamoto ya barabara hii na tutazungumza na wenzetu wa Wizara ya Ujenzi ili tuone namna ya kujenga barabara hii kwa kiwango cha lami na hii itasaidia kuvutia utalii katika maeneo yanayozunguka Hifadhi ya Kitulo.
Mheshimiwa Spika, kwenye suala hili la ujenzi wa ofisi ninaomba nilichukue tukafanye tathmini kuangalia namna iliyo bora ya kufikika kiurahisi, lakini pia kuwepo na hicho kituo ambacho kinawezesha muendelezo wa utalii. Naomba kuwasilisha.
Name
Oliver Daniel Semuguruka
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. FRANCIS L. MTEGA aliuliza: - Je, kuna mpango gani wa kuboresha Hifadhi ya Taifa Kitulo?
Supplementary Question 2
MHE. OLIVER D. SEMUGURUKA, Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana kwa kuniona. Kuna mpango gani wa kuboresha miundombinu ya Hifadhi za Ibanda na Rumanyika zilizopo Wilaya ya Kyerwa ili kuvutia watalii? (Makofi)
Name
Mary Francis Masanja
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Oliver Semuguruka, Mbunge wa Viti Maalum kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, ni kweli tuna hifadhi nyingi ambazo tumeshazitangaza ikiwemo ya Ibanda, Rumanyika, pia Kyerwa. Nimuahidi tu Mheshimiwa Mbunge kwa kuwa Mkakati wa Serikali ni kuhakikisha tuna zindua Phase II ya programu ya Royal Tour. Kwa hiyo, maeneo haya pia tutaweza kuyaingiza ili yaweze kuwa ni ya kimkakati katika kuhakikisha kwamba vivutio hivi tunavitangaza vizuri. (Makofi)
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved