Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Issa Ally Mchungahela
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Lulindi
Primary Question
MHE. ISSA A. MCHUNGAHELA aliuliza: - Je, Serikali ina mkakati gani kuhakikisha uwekezaji wa miradi 294 yenye thamani ya dola bilioni 8.04 inatekelezwa?
Supplementary Question 1
MHE. ISSA A. MCHUNGAHELA: Mheshimiwa Spika, ahsante, ni miradi mingapi ya uwekezaji kati ya hiyo 294 imeanza?
Lakini pili, je, Serikali haioni sababu ya kuanzisha Idara au Kitengo Maalum cha Ufuatiliaji na Ushawishi?
Name
Exaud Silaoneka Kigahe
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mufindi Kaskazini
Answer
NAIBU WAZIRI WA UWEKEZAJI, VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru napenda kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Issa Ally Mchungahela Mbunge, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, kweli katika miradi hii 294 sababu ni swali la takwimu naomba tutafute takwimu zaidi za uhakika na nitampa Mheshimiwa Mbunge ni miradi mingapi ambayo imetekelezwa kati ya hii 294.
Mheshimiwa Spika, kuhusu swali la pili tayari tuna vitengo vya ufuatiliaji kwa maana ya Monitoring and Evaluation katika Wizara, lakini pia hata katika taasisi zetu ikiwemo Kituo cha Uwekezaji cha TIC; na kwa taarifa tu katika miradi ambayo imetekelezwa mwaka 2021/2022 miradi zaidi ya 1,200 imeshafanyiwa ufuatiliaji kwa maana ya kuhakikisha kujua kama inatekelezwa na kwa kiwango gani. Nakushukuru sana.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved