Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Emmanuel Adamson Mwakasaka
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tabora Mjini
Primary Question
MHE. EMMANUEL A. MWAKASAKA aliuliza: - Je, ni lini vibali vya uwindaji vitatolewa?
Supplementary Question 1
MHE. EMANUEL A. MWAKASAKA: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza maswali mawili ya nyongeza. Pamoja na majibu mazuri ya Serikali, nina maswali mawili ya nyongeza.
Mheshimiwa Spika, wafanyabiashara wengi hawa ambao walikuwa wanategemea kuuza nyamapori walishajenga mabucha kwa ajili ya kuuza nyamapori, kama ambavyo Serikali ilikuwa imewahamasisha. Mpaka sasa hivi vibali havijatolewa kwa muda mrefu na hasa kwa hawa wawindaji wa kawaida ambao wanalipa na leseni. Je, Serikali ina mpango gani kuhakikisha kwamba hawa wafanyabiashara wa nyama ya pori wanapata hivyo vibali ili waweze kufungua mabucha yale ambayo walishayajenga?
Mheshimiwa Spika, swali la pili; hata pale nyama hiyo inapokuwa imepatikana kwa hao wachache ambao wanauza, bei yake inakuwa ni ghali sana, na wananchi wengi wa kawaida wangependa kula hii nyama ya porini. Je, Serikali ina mpango gani wa kuweka mazingira mzuri kwa ajili ya kufanya hii nyama ya pori nayo iwe na bei ya kawaida ambapo kila mmoja anaweza kununua? (Makofi)
Name
Mary Francis Masanja
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Emmanuel Adamson Mwakasaka, Mbunge wa Tabora Mjini, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, naomba tu niwatoe wasiwasi Watanzania na Mheshimiwa Mbunge kwamba vibali hivi vitatolewa baada ya mapitio ya Kanuni kukamilika. Tulikuwa na changamoto ya namna ya ugawaji wa vibali hivi kwa kuwa tuliweza kuanzisha makampuni ambayo tuliyakaribisha ili yaweze kuomba vibali vya uwindaji wa kienyeji. Lakini tumegundua changamoto inayojitokeza ni namna ambavyo tunaweza kuwanyima haki ya Kikatiba wananchi kuweza kupata kitoweo ambayo iko ndani ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mheshimiwa Spika, kwa hiyo tumepata maoni kutoka kwa wadau na sasa tumepitia Kanuni hizi, tunatarajia sasa kuzirejesha kwa maana tutoe ile haki ya wananchi, nao wawe na haki ya kuweza kupata kitoweo hiki.
Mheshimiwa Spika, kuhusu bei ya nyamapori, suala hili baada ya kuwa tumepitia Kanuni hizi na wananchi kuruhusiwa nao kuwinda uwindaji wa kienyeji, basi tunatarajia bei ya nyamapori kushuka kuliko ilivyo sasa ambapo tulikuwa tumependekeza makampuni pekee yaweze kuingia katika biashara hii. Ahsante.(Makofi)
Name
Joseph George Kakunda
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Sikonge
Primary Question
MHE. EMMANUEL A. MWAKASAKA aliuliza: - Je, ni lini vibali vya uwindaji vitatolewa?
Supplementary Question 2
MHE. JOSEPH G. KAKUNDA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Kwa kuwa kuna malalamiko mengi sana ya wananchi kwa ajili ya kuruhusiwa uwindaji wa kienyeji, kwa nini Serikali sasa isiharakishe huo mchakato wa mapitio ya Kanuni usiku na mchana ili wiki ijayo waweze kutoa hicho kibali?(Makofi)
Name
Mary Francis Masanja
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Kakunda kama ifuatavyo.
Mheshimiwa Spika, nimtoe wasiwasi Mheshimiwa Mbunge kwamba mchakato umeshakamilika na hivi sasa uko kwenye level ya Waziri, wakati wowote tutaweza kutoa mapendekezo au maelekezo ya utekelezaji wake.(Makofi)
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved